Thursday, October 1, 2020

             2021-MWAKA WA AKILI INAYOPITA MIPAKA

Kingdom Business Clubaship leo Tumeingia Mwaka 2021, Kila Mwaka Tarehe Moja Ya Mwezi Wa 10 Tuna Anza Mwaka MPYA. Tuna Kalenda Yetu Ambayo Tumeipa Majina Kuanzia Siku Mpaka Miaka Kupitia Majina Ambayo Sisi Tuna Fahamu Maana Yake. Tuliona Kutumia kalenda ya Kidunia Siyo Sahihi Na Wala Haina Maana. Hivyo Kalenda Yetu Ni kama ifuatavyo

                    KALENDA YA SIKU 7 ZA WIKI


1. JUMATATU= “Siku Ya Miujiza”

2. JUMANNE= “Siku Ya Hekima”

3. JUMATANO= “Siku Ya Nuru”

4. ALHAMISI= “Siku Ya Matumaini”

5. IJUMAA= “Siku Ya Kristo”

6. JUMAMOSI= “Siku Ya Imani”

7. JUMAPILI= “Siku Ya Ukarimu/Upendo”

                     KALENDA YA MIEZI 12

Majina ya Kalenda ya Mwezi ni kama Ifuatavyo:
1. JANUARY= "Maono"
2. FEBRUARY= "Kibali"
3. MARCH="Uchumi"
4. APRIL="Tai/Kasi/Spidi"
5. MAY="Nyota"
6. JUNE="Ufalme"
7. JULY="Uhuru"
8. AUGUST="Uaminifu"
9. SEPTEMBER="Mavuno"
10. OCTOBER="Kujipa Moyo"
11. NOVEMBER="Shuhuda"
12. DECEMBER="Neema"

                      MAJINA YA MWAKA

Tangu Huduma Hii Ilipoanza Rasmi Tarehe 1/10/2018 Miaka Miwili iliyopita Tumekuwa Na Majina Pamoja Na Maandiko Ya Kusimamia Mwaka Mzima Ni Kama Ifuatavyo:

2018-2019

KAULI MBIU
“The Love of the Truth and in Deed”/ “Upendo wa Kweli Katika Matendo”

NENO LA MWAKA;
Maneno ya Mungu ya Kusimamia yalikuwa “2 Wathesalonike 2:10” pamoja  na “1 Yohana 3:18”

2020

KAULI MBIU
“BE STRONG AND OF GOOD COURAGE”/ UWE HODARI NA MOYO WA USHUJAA

NENO LA MWAKA;
Neno la Mungu la Kusimamia linatoka Katika Kitabu cha Joshua 1:6 ambalo linasema Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana ni wewe utakayewarithisha watu hawa nchi hii niliyowaapia baba zao ya kwamba nitawapa.

                               2021

KAULI MBIU;

THE CROSS OVER MINDSET

            "AKILI INAYOVUKA MIPAKA"

Maelezo Kuhusu Kauli Mbiu hii
Mwaka 2021 Ni Mwaka wa Kuvuka Mipaka Bila Kuwa Na Passport, Vyeti, Kuvuka Mipaka Ya Umaskini, Mipaka Ya Kiuchumi, Ya Kifedha, Mipaka Ya Kiimani...Usikae Mahali Pamoja, Vuka Na Usiridhike Mahali Unapopitia.
Uwe Na Akili Inayovuka Mipaka, Uvuke Mipaka Ya Ugonjwa, Ya Dhambi... Ndiyo Maana Yesu Alipokuja Akasema Tuzaliwe Mara ya Pili-Kuzaliwa Mara Ya Pili Ni Kuvuka Ni Mipaka.

Mwaka Huu 2021 Tutakufundisha Jinsi Gani Ya Kutoka Kuishi Kwenye Nyumba Ya Kupangisha Mpaka Kwenye Nyumba yako Mwenyewe, Kutoka Kuishi Kwenye Nyumba Ya Udongo Mpaka Nyumba Ya Block, Kila Kitu lazima Uende Hatua Ili Uvuke Mipaka Hiyo, Lazima Mungu Akupe Roho Ya Kuvuka Mipaka. 
Kuna Watu Hawasafiri Kabisa Lakini Kwa Mfano Wazungu Wana Safiri Kwa Sababu Wana Roho ya Kuvuka Mipaka Kwenda Nchi Hadi Nchi-Hawaogopi Hata Kama Nchi Hiyo Ina Magonjwa au Vita. Vile Vile Kwa Mfano Tanzania Makabila yenye Roho ya Kuvuka Mipaka ni kama Wamasi na Wachagga! 

Usipo Safari Kuna Mengi Unakosa, Moja Ya Faida Ya Kuvuka Mipaka ni Akili Kuwa Mpya. Kitu Kinacho Safisha Akili Ya Mwanadamu ni KUSAFIRI Mara Kwa Mara Hata Basi Kwa Kutumia Mtandao "Virtue Travel".





NENO LA MWAKA;

MATHAYO 28:16-20
"Na wale wanafunzi kumi na mmoja wakaenda Galilaya mpaka mlima ule aliowaagiza Yesu. Nao walipomwona, walimsujudia; lakini baadhi yao waliona shaka. Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari."

  • "MBINGUNI NA DUNIANI" NI KUVUKA MIPAKA
  • Kuwafanya Watu Kuwa WANAFUNZI WA YESU Ni Kuvuka Mipaka
        MWAKA 2021 NA UWE MWAKA WAKO WA KUVUKA MIPAKA KATIKA MAENEO YOTE YA MAISHA YAKO...

SALAMU YA MWAKA 2021

MWAKA 2021
Caller: YAI FOR CHRIST 2021                                                                                                                
Response: 2021
Caller: YAI FOR CHRIST


Kwa Mawasiliano Zaidi
Mwalimu Bill Mushi , 0788 715656 au 0677 715656
Mtumishi Leonard Kapala, 0769 900401 WhatsApp Group}
Pilot Amanayisye Urassa, 0782 050407 {WhatsApp Group}
                      
                               YESU NI BWANA


Saturday, October 26, 2019

BADILISHA MUDA KUWA AJIRA NA GEUZA AKILI KUWA HEKIMA


JINSI YA KUTENGENEZA AJIRA SEHEMU YA TATU
Salamu!
Yesu Mwana wa Daudi, Hallelujah x3

"BADILISHA MUDA KUWA AJIRA NA GEUZA AKILI KUWA HEKIMA"
UFUNUO WA YOHANA 11:6, MITHALI 3:5, ZABURI 111:10
WARUMI 12:2, 1WAKORINTHO 15:34

Tajirika Na Muda –Tumia Muda Kibiashara
Waefeso 5:15-17, Wakolosai 4:5


Mungu amempa Mwanadamu uwezo mkubwa sana. Mwanadamu anaweza kugeuza Muda kuwa chochote anachotaka kwa kufikiri kwa kina. ‘’Hapo Mwanzo Mungu aliziumba Mbingu na Nchi’’ -Mwanzo ni Muda- ‘’KUTAFAKARI’’
ZABURI1:1-3 JOSHUA 1:8 UFUNUO 11:6

Mwanadamu anaweza kugeuza akili kuwa pesa. Mungu alimpa Sulemani Hekima akaigeuza akili kuwa Utajiri.
Kugeuza akili kuwa Hekima ni kubadili akili kuwa vitu. Mawazo ni vitu Geuza Mawazo yako kuwa Sayansi ,Tekinolojia Ufundi, Vitabu, Semina, Sinema na DVD;s, CD’s nk.

Hekima ni kitu cha mwisho, ukiona Magari ya aina ya Toyota ni Hekima ya MJAPANI – ‘’Japanese Wisdom’’.

Katika Roho Saba za Mungu, Nne zinahusiana na Hekima. Roho ya ufahamu ni Hekima, Roho ya Ushauri ni Hekima, Roho ya Maarifa ni Hekima na Roho ya Hekima ni Hekima. Ukigeuza Akili kuwa Hekima huwezi kushindwa mahali popote Duniani na Mbinguni-ISAYA11:2

Ukitengeneza ajira kivuli utapata faida kivuli na faida kivuli inatengeneza faida hasili. Ajira kivuli ni kazi za Kijamii, Ukipanda Mbegu ya Kazi utavuna Matunda ya Kazi. Ajira ni kama nyumba huwezi kujenga nyumba bila kuwa na Ramani ya jengo. Ramani ni nyumba kivuli.

Anza kidogo kidogo mwenyewe na Muda wako wa masaa 24Hrs mpaka ufikie kiwango cha Kugeuza Muda kuwa Ajira. Wewe unafikiri wengine wanafanya kazi.

Ajira kivuli ndiyo jibu la kila Mtanzania na Dunia kwa ujumla. Ramani ya Ajira ni kazi za kijamii-MATHAYO 6:33

Ajira kivuli ni Kazi ya Yesu, Kazi ya Adamu na Kazi ya Injili.
Kazi ya Yesu ni kusaidia Yatima,Wajane, Wafungwa, Wagonjwa, Watoto wa Mitaani,Walemavu, Wazee na Wasio jiweza.

Kazi ya Adamu ni Kutunza Mazingira, Wanyama, Misitu na Vyanzo vya Maji.

Kazi ya Injili Kufundisha Habari Njema.

KUMBUKA KWA MUNGU HAKUNA KUJITOLEA ANALIPA KILA BAADA YA DAKIKA SITINI. "60MINS"-LISAA LIMOJA’, UNAMCHAJI MUNGU KWA KILA LISAA LIMOJA KIWANGO UNACHOTAKA KULINGANA NA UZITO WA KAZI UTAKAYO FANYA-MATHAYO 20:1-16

Kama unahitaji kazi lazima utembee kwenye agano la kazi upande Mbegu ya kazi uipe muda utavuna matunda ya kazi yako. Kila kitu unachokiona Duniani kina Mbegu, nikikupa Tsh 1000 Sasa hivi kuna mbegu ndani yake asilimia moja ambayo ni Tsh Shilling kumi-MWANZO 8:22

Ukiona Wazungu wana kuja Afrika kufanya kazi za kijamii kama kwenye Vituo vya Watoto Yatima, Mashule, Hospitali, Kutunza Mazingira, NGO’s mbalimbali wamekuja kupanda mbegu ya kazi. Mungu anataka umuonyeshe kazi ya mfano ili aweze kukutengenezea Ajira.

Kazi ya Muda ni Kufikiri, Kutengeneza Ajira, Wazo la Biashara na Kutafuta Taarifa. Kazi ya Muda siyo kutafuta pesa, Kazi ya pesa ni kuukomboa Muda wako. Kwa mfano Safari ya kutoka Arusha mpaka Dar ess salaam kwa Basi ni masaa kumi , ukisafiri kwa Ndege ni lisaa limoja kwahiyo ukipanda Ndege utakuwa umekomboa masaa tisa, Hiyo ndiyo kazi ya pesa, WAEFESO 5:15-17, WAKOLOSAI 4:5

Mimi nimebadili Muda wangu kuwa ajira na nimegeuza Akili yangu kuwa Pesa. Kila mtu anaweza kufanya kama nilivyo fanya mimi, 1 WAKORINTHO 15:34

Ajira yako ipo ndani ya Muda wako na pesa zako zipo ndani ya akili yako kila mtu anao Muda wa masaa 24hrs na kila mtu anazo akili. Akili haitengenezi Pesa mpaka ibadilike kuwa Hekima. Sulemani alitatua matatizo ya watu kwa kutumia Hekima. Mfalme Sulemani hakutatua Matatizo kwa kutumia Pesa kama Dunia ya Leo walio wengi wafanyavyo. Utakapotatua tatizo la mtu kwa muda wako na akili yako atakulipa.

Akili ni rafiki mkubwa wa muda mahali akili yako itakapo kwenda ndiko muda wako utakapo kwenda, kitakachomea kwenye Ubongo ndicho kitakachomea kwenye moyo wako, MITHALI 23:7 MATHAYO 6:19-21

Kazi ya Akili ni kuuza Muda kwa Faida, Akili ikishindwa kuuza Muda mtu huyo basi anaitwa Maskini. Mungu na wanadamu wote wananunua Muda. Mungu analipa vizuri kuliko wanadamu. Mungu ni mwaminifu sana na analipa wakati huo huo ukimaliza kazi yake.

Watu wengi hawajui mfumo wa Mungu anaotumia kuwalipia watu wanao mtumikia katika ufalme wake. Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika Roho na kweli. Watu wanajua mifumo ya kimwli tu hawajui mifumi ya kiroho. Aliyezaliwa kimwili analipwa kimwili aliyezaliwa kiroho analipwa kiroho, YOHANA 4:24 , YOHANA 3:6.

Mifumo ya Mungu ya malipo ipo hapa katika maandiko yasemayo’’ Kwa sababu Mungu humpa yeye aliyemrithia Hekima, Maarifa na Furaha; bali mwenye dhambi au mkosaji humpa taabu ili kukusanya na kututa au kurundika apate kumpa huyo ambaye Mungu amrithia’’- MHUBIRI 2:26, PIA KUTOKA 23:25-25, AYUBU 36:11, MATHAYO 6:33. YOHANA 15:16, ISAYA 3:10

SEHEMU HII NI YA MAANDIKIKO MATAKATIFU:
“Hao wana amri ya kuzifunga mbingu, ili mvua isinyeshe katika siku za unabii wao. Nao wana amri juu ya maji kuyageuza kuwa damu, na kuipiga nchi kwa kila pigo, kila watakapo.” SUV UFUNUO WA YOHANA 11:6,

“Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;” SUV MITHALI 3:5,
“Kumcha Bwana ndio mwanzo wa hekima, Wote wafanyao hayo wana akili njema, Sifa zake zakaa milele.” SUV ZABURI 111:10
“Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
” SUV WARUMI 12:2,
“Tumieni akili kama ipasavyo, wala msitende dhambi; kwa maana wengine hawamjui Mungu. Ninanena hayo niwafedheheshe.” SUV 1 WAKORINTHO 15:34

“Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu. Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana” SUV WAEFESO 5:15-17,

“Enendeni kwa hekima mbele yao walio nje, mkiukomboa wakati.” SUV WAKOLOSAI 4:5
“Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana” SUV JOSHUA 1:8
“Na roho ya Bwana atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha Bwana;” SUV ISAYA 11:2

“Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.” SUV MATHAYO 6:33

“Muda nchi idumupo, majira ya kupanda, na mavuno, wakati wa baridi na wakati wa hari, wakati wa kaskazi na wakati wa kusi, mchana na usiku, havitakoma.” SUV MWANZO 8:22
“Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo. Akuambia, Haya, kula, kunywa; Lakini moyo wake hauwi pamoja nawe.” SUV MITHALI 23:7

“Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.” SUV YOHANA 4:24 ,

“Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.” SUV YOHANA 3:6
“Kwa sababu Mungu humpa yeye aliyemridhia hekima na maarifa na furaha; bali mkosaji humpa taabu, ili kukusanya na kututa, apate kumpa huyo ambaye Mungu amridhia. Hayo nayo ni ubatili na kujilisha upepo.” SUV MHUBIRI 2:26,

“Kama wakisikia na kumtumikia, Watapisha siku zao katika kufanikiwa, Na miaka yao katika furaha” SUV AYUBU 36:11,
“Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni.” SUV YOHANA 15:16,

“Waambieni wenye haki ya kuwa watakuwa heri, kwa maana watakula matunda ya matendo yao” SUV ISAYA 3:10

SALA YA YA TOBA
YESU MWANA WA DAUDI…X3
Mimi “Taja Majina yako Mawili”
NAOMBA UNIREHEMU…X3
Unisamehe Makosa Yangu Yote,
 Unisamehe Dhambi Zangu Zote,
Unisamehe Maovu Yangu Yote,
Uniponye na Magonjwa Yangu Yote
Unisafishe Kwa Damu Yako Takatifu,
Kuanzia Leo,
Ninakiri,
Nimekua Kiumbe Kipya,
Ya Kale Yamepita,
Futa Jina Langu,
Katika Kitabu Cha Mauti,
Andika Jina Langu Katika,
Kitabu Cha Uzima,
Asante Mungu,
Kwa Kunipenda,
Asante Yesu Kristo,
Kwa Kuniokoa,
Asante Roho Mtakatifu,
Kwa Kunifundisha,
Asante Malaika Wa Mungu,
Kwa Kunilinda,
Katika Jina la Uweza la
YESU KRISTO wa Nazareti.
*AMEN*

JIBARIKI MWENYEWE
HAKIKA, MIUZIJA YA KRISTO,
ISHARA NA MAAJABU,
ZITA NIFUATA MIMI,
“TAJA MAJINA YAKO MAWILI”
SIKU ZOTE ZA MAISHA YANGU,
NAMI NINA KAA NYUMBANI MWA BWANA,
MILELE NA MILELE.
*AMEN*

MASOMO HAYA YANATOLEWA BURE KATIKA OFISI ZETU ZA ARUSHA WASILIANA NASI
 +255 788 71 56 56

SHIRIKISHA WENGINE  BARAKA HIZI  UPATE KUBARIKIWA NA WEWE.
                                               MWANZO 12:1-3


Thursday, October 24, 2019

JINSI YA KUTENGENEZA AJIRA SEHEMU YA PILI

Salamu!
Yesu Mwana Wa Daudi, Hallelujah x3

FANYA KAZI KWA MUDA SIYO KWA MIKONO
2 WAKORINTHO 5;7

Tajirika Na Muda - Tumia Muda Kibiashara
Waefeso 5:15-17

Kufanya Kazi Kwa Muda Na Siyo Kwa Mikono Maana Yake Kufanya Kazi Kwa Kutumia  Muda Wako Mwenyewe Wa Masaa 24Hrs Na Kutumia Muda Wa Watu Wengine.  Huwezi Kutajirika Kwa Masaa Yako 24hrs Tu Bali Kwa Kutumia Muda Wa Watu  Wengine.

Ili Uwe Na Muda Zaidi Ya Masaa 24Hrs Chukua Masaa 10Hrs Ya Watu Wengine Kumi(10x10=100) Jumlisha Na Ya Kwako 24Hrs Utakuwa Na Masaa 124Hrs Kwa Siku,  Siyo Masaa 24Hrs Kama Watu Wa Kawaida. UTAJIRI UPO KWENYE MUDA SIYO KWENYE PESA.   
‘’Foolish people use heart to think, But Smart people use brain to think’’.

Tasfiri Ya Kazi Ya Muda Ni Kufikiri, Kutengeneza Ajira, Wazo La Biashara Na Kutafuta Taarifa Kama Vile Unavyosoma Taarifa Hizi.

Wazungu Wanapigana Na Vita Vya Ujinga, Waafrika Wengi Sana Wanapigana Na  Vita Vya Umaskini’. Ukisikia Mtu Ana Kwambia Yule Bwana Ni Mzungu Kwasababu Anatumia Muda Vizuri Anachokisema Ndicho Anachokifanya, Akikuambia Ni Mswahili Basi Kuna Changamoto Hapo. UKISEMA JAPAN UNASEMA MUDA UKISEMA AFRIKA UNASEMA PESA.

Watu Wote Waliofanikiwa Duniani WALIFANYA KAZI ZA MUDA NA SIYO ZA MIKONO! Kuna Aina Mbili Za  Kazi Hapa  Duniani; Kazi Za Muda Zinahitaji Kufikiri Sana.  Kuajiriwa Siyo Kitu Kibaya Bali Ujue Umenyanganywa Uwezo Wa Kufikiri Asilimia 98%.

  •  AKILI KAZI –KUJIAJIRI-  Mungu Anabariki Kazi Ya Akili Yako. 1 KOR 15:34
  •   MKONO KAZI-KUAJIRIWA-Mungu Anabariki Kazi Ya Mkono Wako. KUMB. 28:12

Kazi Zote Zinazofanywa Na Akili Zinafanywa Kwa Muda Na Zile Zinazofanywa Kwa Mikono Zinafanya Kwa Nguvu . Kwa Kuwa Kazi Zote Za Akili Hazi Hitaji Nguvu Wala Vyeti Vya  Chuo Bali Zina Hitaji Muda Tu. Ajira Unayotafuta Leo Ni Ya Aina Gani? Je, Ni Ya Kutumia Muda Au Kutumia Mikono?

Kazi Ya Akili  Unaanzisha Mwenyewe Kwa Kufiri Kwa Kina.Na Hauhitaji Vyeti Ni Ubunifu Tu, Katika Huduma Hii Ya Kingdom Business Clubship Tuna Kufundisha Matumizi Ya Muda Wako Katika Kazi Zote Mbili Kazi Ya Akili Na Kazi Ya Mikono. Kazi Ya Akili Ni Kujiajiri Mwenyewe, Na Kazi Ya Mikono Ni Kuajiriwa. Utakapo Anza Kufikiri Kila Kitu Mwenywe Na Kutumia Akili Yako Asilimia Mia Moja.

Meneja Wa Benki Anatumia Akili Yake Asilimia Mbili Tu  Mama Anayechoma Mahindi Anatumia Akili Yake Asilimia Mia Moja, Kwa Kutafuta Masoko, Kujali Wateja, Matangazo, Nk. Mama Huyu Anafanya Hivi Vyote Mwenyewe. Na Yule Meneja Wa Benki Amerahisishiwa Vitu Kwani Kuna “System” Mfumo Wa Kila Kitu Anakikuta Kazini.

AKILI KAZI NA MKONO KAZI  Ni Kufikiri Kwa Matendo, Yaani Unafikiri Huku Unafanya Hii Ndiyo Njia Peke Yake Inaweza Kumtoa Mtu Katika Umaskini. Muda Unapewa Na Mungu Pesa Unatafuta Mwenyewe, Mungu Anakupa Unachokiitaji, Hakupi Unacho Kitaka. Unahitaji Muda Kutafuta Unacho Kitaka. 1 WAFALME 3:5, MITHALI 30:7-9        

MWISHO WA SEHEMU YA PILI

SEHEMU HII NI YA MAANDIKIKO MATAKATIFU:
“kwa maana twaenenda kwa imani wala si kwa kuona.” NEN 2 WAKORINTHO 5:7

“Kwa hiyo iweni waangalifu jinsi mnavyoenenda, si kama watu wasio na hekima, bali kama wenye hekima, 16mkiukomboa wakati, kwa sababu nyakati hizi ni za uovu. Kwa hiyo msiwe wajinga, bali mpate kujua nini yaliyo mapenzi ya Bwana.” NEN  WAEFESO 5:15-17

“Zindukeni mwe na akili kama iwapasavyo, msitende dhambi tena, kwa maana watu wengine hawamjui Mungu. Nasema mambo haya ili mwone aibu.” NEN 1 WAKORINTHO15:34

“BWANA atafungua mbingu, ghala zake za baraka, kukupa mvua kwa majira yake na kubariki kazi zako zote za mkono Wako. Utakopesha mataifa mengi lakini hutakopa kwa ye yote.” NEN KUMBUKUMBU LA TORATI 28:12

 “BWANA akamtokea Solomoni huko Gibeoni wakati wa usiku katika ndoto, naye Mungu akasema, ‘‘Omba lo lote utakalo nikupe.’’  NEN 1 WAFALME 3:5

“Ninakuomba vitu viwili, Ee BWANA, usininyime kabla sijafa: Uutenge mbali nami udanganyifu na uongo, usinipe umaskini wala utajiri, bali unipe chakula cha kunitosha kila siku. Nisije nikawa na vingi vya kuzidi nikakukana na kusema, “BWANA ni nani?’’ Au nisije nikawa maskini nikaiba, nami nikaliaibisha jina la Mungu wangu” NEN MITHALI 30:7-9

MASOMO HAYA YANATOLEWA BURE KATIKA OFISI ZETU ZA ARUSHA WASILIANA NASI +255 788 71 56 56

SHARE, “WATUMIE NA WENGINE UJUMBE HUU WAPATE KUJIFUNZE NA WAO”.


Tuesday, October 22, 2019

JINSI YA KUTENGENEZA AJIRA SEHEMU YA KWANZA

Salamu!

Yesu Mwana wa Daudi, Hallelujah x3

JE! UNASHAUKU NA NIA YA KUFANYAKAZI? JE! UNAMAONO YA AJIRA?
“Kwa maana hata tulipokuwa pamoja nanyi, tuliwapa amri ili kwamba: ‘‘Mtu ye yote asiyetaka kufanya kazi, wala asile.’’ Kwa kuwa tunasikia kwamba baadhi ya watu miongoni mwenu ni wavivu. Hawafanyi kazi bali hujishughulisha na mambo ya wengine. Basi watu kama hao tunawaagiza na kuwaonya katika Jina la Bwana Yesu Kristo wafanye kazi kwa utulivu na kujipatia mahitaji ya maisha yao wao wenyewe.” 2 WATHESALONIKE 3:10-12
 “Kwa maana viumbe vyote vinangoja kwa shauku kudhihirishwa kwa watoto wa Mungu.” WARUMI 8:19

TAFUTA MAKAMPUNI BINAFSI MATATU, MASHIRIKA YA KIMATAIFA, NGO’S, TAASISI ZA UMA, AU SEREKALINI.
“Ombeni nanyi mtapewa, tafuteni nanyi mtapata, bisheni nanyi mtafunguliwa mlango. Kwa maana kila aombaye hupewa, naye atafutaye huona, naye abishaye hufunguliwa mlango.” MATHAYO 7:7-8

 ‘ANDIKA BARUA ZA MAOMBI YA KAZI SEHEMU TATU TOFAUTI, AMBATANISHA NA WASIFU WAKO “CV’S”.
“Nitasimama katika zamu yangu na kujiweka mwenyewe juu ya maboma, Nitatazama nione atakaloniambia na    ni jibu gani nitakalotoa kuhusu lalamiko hili. Jibu La BWANA Kisha BWANA akajibu: Andika ufunuo huu na ukaufanye wazi juu ya vibao ili mpiga mbiu akimbie nao. Kwa kuwa ufunuo huu unasubiri wakati uliokubalika, unazungumzia mambo ya mwisho na kamwe hautakosea. Iwapo utakawia, wewe usubiri, kwa hakika utakuja na hautachelewa.”HABAKUKI 2:1-3.

CHUKUA HATI YA TABIA NJEMA KUTOKA POLISI.
Msidanganyike, “Ushirika na watu wabaya huharibu tabia njema.” 1 WAKORINTHO 15:33

PELEKA MAOMBI YAKO YA AJIRA KWA MCHUNGAJI WAKO AU KIONGOZI WAKO WA IMANI AYABARIKI..  
“Mungu akawabariki na akawaambia, “Zaeni na mkaongezeke, mkaijaze tena dunia na kuitiisha. Mkatawale samaki wa baharini, ndege wa angani na kila kiumbe hai kiendacho juu ya ardhi.’’ MWANZO 1:28
“Mungu akaibariki siku ya saba akaifanya takatifu, kwa sababu katika siku hiyo alipumzika kutoka kazi zote za kuumba alizokuwa amefanya.” MWANZO 2:3
NENDA UKAFANYE KAZI KIMVULI KATIKA VITUO VYA WATOTO YATIMA ,WAJANE, WAZEE, WATOTO WA MITAANI, KUTEMBELEA WAFUNGWA KUWATIA MOYO, KWANDA HOSPITALINI KUOMBEA WAGONJWA, KUTUNZA MAZINGIRA, NA KUHUBIRI INJILI, CHAGUA KAZI MOJA TU KATIKA HIZO HAPO JUU.
“Dini iliyo safi, isiyo na uchafu, inayokubalika mbele za Mungu Baba yetu, ndiyo hii: Kuwasaidia yatima na wajane katika dhiki zao na kujilinda usitiwe madoa na dunia.” YAKOBO 1:27

“BWANA Mungu akamchukua huyo mtu akamweka kwenye Bustani ya Edeni ailime na kuitunza” .MWANZO 2:15

“Kwa maana nilikuwa na njaa mkanipa chakula, nilikuwa na kiu mkaninywesha, nilikuwa mgeni mkanikaribisha, nilikuwa uchi mkanivika, nilikuwa mgonjwa mkanitunza, nami nilikuwa kifungoni mkaja kunitembelea” MATHAYO 25:35-36
“Basi wale wanafunzi kumi na mmoja wakaenda hadi Galilaya kwenye ule mlima ambao Yesu alikuwa amewaagiza. Walipomwona, wakamwabudu, lakini baadhi yao wakaona shaka. Yesu akawajia na kusema, “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Kwa sababu hii, enendeni ulimwenguni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, nanyi wafundisheni kuyashika mambo yote niliyowaamuru ninyi. Hakika Mimi niko pamoja nanyi sikuzote, hadi mwisho wa nyakati.’’ Amen.  MATHAYO 28:16-20


ANZA MAOMBI YA KUOMBEA WATU AMBAO HAWANA KAZI WAPATE KAZI KWA KUSIMAMIA ANDIKO HILI
“Baada ya Ayubu kuwaombea rafiki zake, BWANA akamfanikisha tena naye akampa mara mbili kama yale aliyokuwa nayo hapo kabla.” AYUBU 42:10


INGIA KWENYE MAOMBI YA TOBA NA REHEMA MARA SABA KWA SIKU 
“Baba Jehovah akusamehe dhambi zako zote  na kuponya magonjwa yako yote, kwa Damu ya Yesu kristo, Kwa maana fadhili zake niza milele katika   jina la Yesu kristo wa Nazareth”  ZABURI 103:3
 “Ee Mungu, unihurumie, kwa kadri ya upendo wako usiokoma  kwa kadri ya huruma  wako usiokoma,yako kuu uyafute makossa yangu yote kwa Damu ya Yesu kristo, Kwa maana fadhili   zake niza milele katika   jina la Yesu kristo wa Nazareth,” ZABURI 51:1

UTAKAPOKUWA UNAJIANDAA KWENDA KATIKA USAILI SIMAMIA MAANDIKO HAYA
‘‘Watakapowapeleka katika masinagogi mbele ya watawala na wenye mamlaka, msiwe na wasiwasi kuhusu namna mtakavyojitetea au mtakavyosema: Kwa maana Roho Mtakatifu atawafundisha wakati uo huo mnachopaswa kusema.” LUKA 12:11-12

ANZA KUMSHUKURU MUNGU KWA KUPATA AJIRA KILA BAADA YA DAKIKA SITINI LISAA LIMOJA. MUNGU NI ALPHA NA OMEGA 59MINS-60MINS
“Shukuruni kwa kila jambo, kwa  maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu kwa ajili yenu katika Kristo Yesu.” 1 WATHESALONIKE 5:18

MASOMO HAYA YANATOLEWA BURE KATIKA OFISI ZETU ZA ARUSHA WASILIANA NASI +255 788 71 56 56

SHARE, “WATUMIE NA WENGINE UJUMBE HUU WAPATE KUJIFUNZE NA WAO”.



Monday, October 21, 2019

FORMULA YA UJASIRIAMALI, MAISHA, BIASHARA NA HUDUMA (FORMULA 0-9)


Salamu
Yesu Mwana Wa Daudi, Hallelujah X3

FORMULA YA UJASIRIAMALI, MAISHA, BIASHARA NA HUDUMA (FORMULA 0-9)
 ANDIKO KUU: Mithali 3:13-20 “19-20”
"Kwa hekima BWANA aliiweka misingi ya nchi;
Kwa akili zake akazifanya mbingu imara;
Kwa maarifa yake vilindi viligawanyika;
Na mawingu yadondoza umande"

MAANDIKO MENGINE: Methali 2:1-22, 4:7, 23:23. Yakobo 1:5, 3:15-17, Isaya 11:2


Watu Wote Wajanja Duniani Walifudishwa Kuhesabu Kuanzia 0-9(Watu Hawa Walikuja Duniani Kama MBEGU "Walitengenezwa Kama Mbegu"-LUKA 8:11). Watu Wa Aina Ya Pili Walikuja Duniani Kama MKATE Ambao Walifundishwa Kuhesabu 0-100(Mashuleni, Vyuoni, Walitengenezwa Pia!!!

Ukiangalia Vifaa Vyote Duniani Vya Mashine “Analog Or Digital Machines” Zimewekwa Namba 0-9, Angalia Simu Yako Sasa Hivi Ina Namba Ngapi?= 0-9

Kikokotozi Cha Mahesabu Yote Duniani “Calculator” Hupigwa Kwa Namba Hizi Tu 0-9. Hivyo Basi Jifunze Leo Kwa Mtiririko Huu (Ufuatao) NA HUTAKIWI KURUKA HATA NAMBA MOJA(Utapata Ajali). Unatakiwa Siku Zote Uanze Na "0" KWENDA "9"...Hata Gari Huanza Na Spidi 0.

FORMULA 0-9
0-LOVE/UPENDO=1 Kor 13:8, Luka 10:27, 1 Yohana 3:18, Wim 8:6, Yohan 3:16, Gal 5:22-23
1-TIME/MUDA= Mwa 1:1, Efe 5:16, Kol 4:5, Yn 5:17, Mhu 3:1
2-INFORMATION/TAARIFA=Isa 34:16, Yoh 1:8, Efe 1:17-18
3-KNOWLEDGE/MAARIFA=Yer 3:15, Hos 4:6, Isa 5:13
4-UNDERSTANDING/UFAHAMU=Mit 3:13, Mit 13:15
5-FAITH/IMANI= Rum 10:17, Ebr 11:1-6, Gal 5:6
6-WISDOM/HEKIMA= Isa 11:2, Yak 3:17, Yak 1:5, Mit 24:3-6, Mit 3:19-20, 1Kor 3:6-7
7-PEOPLE/WATU= Mt 4:19, Yn 21:15-17, Mit 11:30, 2 Pet 3:9
8- CASH/FEDHA A.K.A MONEY/PESA=Mt 6:24, 1Tim 6:10, Efe 5:5, Mit 23:4, Mit 28:22
9-THINGS/VITU"UTAJIRI"= Mt 6:33, Kut 23:25-26, Ayu 36:11, Isa 3:10, Yn 15:16, 2 Nya 9:1-12, Mwa 13:2, Mwa 24:35, Zab 112:3, Mit 10:22

UFAFANUZI WA FORMUAL 0-9
Chochote Unachokita Duniani Unaweza Kukipata Hata Kama Ni KIPAWA AU SKILLS!!!

TALENT/GIFT “KIPAWA”
Kipawa (KUJIFUNZA KUPITIA MAZOEZI/PRACTICAL) Ni ZAWADI Kutoka Kwa MUNGU. Lakini Mimi Nasema Ukitumia “0-9 Formula” Kwenye Jambo Fulani au Lolote Lile Pia Ukitafuta KIPAWA CHOCHOTE KILE LAZIMA UTAKIPATA YAANI MUNGU ATAKIWEKA KIPAWA HICHO MIKONI MWAKO-KItabu Cha Kutoka 31:1-5 (Mtu Huyu Anaenenda Kwa Imani “Mind Sight”

SKILLS “UJUZI”
Ujuzi(Mimi nauita KUJIFUNZA KUPITIA THEORY-Makaratasi tu) Una Patikana Kupitia Shule/Chuo. Mtu Anayehitaji UJUZI Ni Kwa Ajili Ya Kutafuta Ajira Aajiliwe... Yaani Apate Cheti, Mtu Huyu anaenenda kwa Kuona “Eye Sight”.

MCHANGANUO WA 0-9
0=UPENDO, Ukikipenda Kitu Chochote Duniani UKIKIPENDA Utakipa 1=MUDA, {Kazi Ya Muda Ni Kufikiri, Kutengeneza Mawazo Mapya Na Kutafuta Taarifa} Kwa Hivyo Ukitoa tu Muda Wako Kile Kitu Kitakuletea 2=TAARIFA, Taarifa Zikizidi Zitakuletea 3=MAARIFA, Maarifa Yakizidi Kwa Wingi Yatakuletea 4=UFAHAMU {Watu Wengi Sana Hufanya Vitu Pasipo UFAHAMU, Ukiona Kwenye Biblia Pameandikwa UFAHAMU Maana Yake ni AKILI, -Akili ya Mtu Haikui Kwa Umri INAKUWA KWA TAARIFA UNAZOPATA.
KWA HIVYO 4=UFAHAMU Ukizidi/Ukiongezeka Ndipo 5=IMANI Inaingia{Soma Maandiko Pale Juu KUHUSU IAMANI}. ILI IMANI YAKO IKAMILIKE LAZIMA IWE NA VITU VITATU
a) ZAO LA IMANI Mf. Rozari ya Katoriki, MAJI YA HUDUMA MBALIMBALI, STICKERS ZA HUDUMA n.k
b) HUDUMA YA IMANI Mfano Kutembelea Na Kusaidia  YATIMA “KWENDA KUFANYANYA KAZI YA YAI”
c) NENO LA IMANI “ Your KEYWORD”, Neno La Kusimamia

Imani Yako Ikizidi Ndipo 6=HEKIMA inazaliwa Sasa. Hekima ni nini? HEKIMA NI KITU CHA MWISHO KABISA. Hekima Inaonekana Kwa Wanadamu Kupitia Vitu Wanavyo Tengeneza Kwa Magfano Utaona Mtu Anatengeneza Kitu Kwa Ubora Wa Hali Ya Juu Ambapo Hakuna Mtu Mwingine Duniani Anacho(KIPAWA) Ana Mtumia SANA MUNGU wa OMEGA “FINISHING GOD” {Ufu 1:8}

BADO TUPO KWENYE 6=HEKIMA, Mfalme Sulemani Alianza na 0=UPENDO "Sulemani naye akampenda Mungu"= 1 Fal 3:3, Sulemani Alilipa DENI LA Upendo kwa Mungu  KWANZA na Mungu akampa HEKIMA(Hekima ya Uongozi)
HEKIMA ikizidi Unaipeleka kwa 7=WATU, Watu Watakupa 8=FEDHA. Kuna tofauti Kati FEDHA/CASH na MONEY/PESA. Pesa ni ROHO na Fedha ni FEDHA TASLIM Tunaziona Kupitia Noti Na Safaru. FEDHA ikija sasa wewe unanunua 9=VITU, UTAJIRI unaingia.

Jiulize Unafuata Hivi?
Sasa Watu Wengi Sana Huanza KWA KASI Kutafuta Namba 8=FEDHA Moja Kwa Moja Wakati Hawana Vitu Vya Mwanzoni UPENDO-MUDA-TAARIFA-MAARIFA-UFAHAMU-IMANI-HEKIMA-WATU Ndio ije FEDHA. Fedha ndiyo BIASHARA YA KWANZA Kuifanya na vile vile Ndio BIASHARA YA MWISHO KUIFANYA

Utakuta Ukimpigia mtu Simu Kwa Mara Ya Kwanza au Ukakosea Kutuma SMS Utakuta anakutumia SMS au Ana Kupigia Simu anakuuliza "WEWE NANI" BADALA Alitakiwa Akuulize, “Habari za saa Hizi, Samahani Naona Imekuja tu Namba bila Jina, Napenda Kukufahamu Sijui Mwezangu Nani?” BADALA YAKE NANI WEWE Unajua Maana Yake Nini Msemo Huu?
1.ANA HASIRA, AMEUDHIWA HUKO ANA KULAUMU WEWE
2."MIMI SIPENDI WATU" Maana yake USINISUMBUESUMBUE,
3.TABIA YANGU SI NJEMA NAPENDA KUKAA MWENYEWE Wakati Huku Ana Sema Biashara Ngumu Na huku Hapendi Watu. Jifunze KUZUNGUMZA Pamoja Na KUANDIKA LUGHA NZURI KWENYE SIMU.

HITIMISHO
“Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki.”  SUV YAKOBO 3:17 

SHARE HII, “WATUMIE NA WENGINE UJUMBE HUU WAPATE KUJIFUNZE NA WAO”.

Thursday, October 10, 2019

2020-Mwaka wa Uhodari, Ujasiri na Moyo wa Ushujaa

YESU MWANA WA DAUDI X3
Habari za leo Mwana wa Mungu, Kila Tarehe 1,ya mwezi wa 10, Huduma hii ya KINGDOM BUSINESS CLUBSHIP Duniani huanza na Mwaka Mpya, KWA HIVYO KILA TAREHE 1 MWEZI WA 10 NDIYO MWAKA MPYA WETU. Kwa kusema hivyo basi tulianza mwaka MPYA-2020 tarehe 1 mwezi huu. Tunapoanza mwaka huduma hutoa Neno Na Kauli mbiu ama kwa lugha ingine NENO LA KUTEMBEA NALO MWAKA MZIMA. Kwa mfano tulianza mwaka jana 2018-2019 mwezi wa 10 tarehe 1 na:

MWAKA 2019 Tulikuwa na Neno Linalosema
KAULI MBIU;
Caller: YAI FOR CHRIST 2019
Response: 2019
Caller: YAI FOR CHRIST


NENO LA MWAKA MZIMA LILIKUWA;
“The Love of the Truth and in Deed”/ “Upendo wa Kweli Katika Matendo”
Maneno ya Mungu ya Kusimamia yalikuwa “2 Wathesalonike 2:10” pamoja  na “1 Yohana 3:18”

Oktober 1 tuliingia mwaka mpya 2020, Na Neno la mwaka huu linasema
“BE STRONG AND OF GOOD COURAGE”/ “UWE HODARI NA MOYO WA USHUJAA”
Pia tuliondoka kwenye kutumia kalenda ya kidunia kwa kuanza kuzipa majina SIKU, MWEZI NA MWAKA tangia mwisho wa mwaka jana. Mwezi huu wa 10 ninyi mmeuzoea kuita OCTOBER ila sisi tumeupa jina la THE COURAGE yaani UJASIRI au USHUJAA hivyo namba 10 kwetu sisi ni Ushujaa kwako Wewe je unauhitaje? Bado miezi miwili tukamishe Kalenda yetu yam waka mzima.

MWAKA 2020 Neno linasema;
KAULI MBIU:
Caller: YAI FOR CHRIST 2020                                                                                                                
Response: 2020
Caller: YAI FOR CHRIST


NENO LA MWAKA;
“BE STRONG AND OF GOOD COURAGE”/ UWE HODARI NA MOYO WA USHUJAA”
Neno la Mungu la Kusimamia linatoka Katika Kitabu cha Joshua 1:6 ambalo linasema Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana ni wewe utakayewarithisha watu hawa nchi hii niliyowaapia baba zao ya kwamba nitawapa.

Caller(Mtu akikwambia): 2020
Response(Unajibu): “Be Strong and of Good Courage” au "Uwe Hodari na Moyo wa Ushujaa"

Mungu alimwambia Yoshua “Uwe Hodari na moyo wa ushujaa”- Usiogope. Mungu alirudia kumwambia Yoshua mara 7 awe Hodari na moyo wa Ushujaa. Kukiwa kuna moyo mzuri wa ushujaa(hutoka kwa Mungu) ujue pia kuna MOYO MBAYA WA USHUJAA PIA(yaani namna ya kupenda fedha/Mali/dunia hii). Kuna mfano wa watu wa aina mbili hapa ambao wote walikuwa ni MAJUSHAA. Rais Mtaafu wa Afrika ya Kusini NELSON MANDELA alikuwa na MOYO MZURI WA USHUJAA lakini tuna Mwingine Dikteta Adolph Hitler alikuwa na MOYO MBAYA WA USHUJAA.
Swali kwako, Je wewe una moyo wa aina gani katika Maisha unayopitia hivi leo? Ni kitu gani kina kuogopesha ya kwamba watu au jamii ikijua utafadhaika sana? Ni wapi Umekosa Ujasili au umekwama? TUANDIKIE SMS AU COMMENT HAPO CHINI

Kwa Mawasiliano Zaidi
Mwalimu Bill Mushi , 0788 715656 au 0677 715656
Mtumishi Leonard, 0756 877161 au 0621 133985
Pilot Ami, 0782 050407{WhatsApp Group}
                      
                               YESU NI BWANA


Tuesday, February 6, 2018

Mistari Ya Toba



                KINGDOM BUSINESS{Mathayo 6:33}                         
                                MISTARI YA TOBA
1.Anza kwa Shukrani=Zaburi 100:4, Zaburi 116{12-19}*17 mpaka Zab.118<zote>
2.Zaburi 51:1-19,  Unaweza Rudia x1,x3,x7,x10,x12
3.Zaburi 103:3{Gazeti la Lisaa-Tamka Kila Lisaa Siku 7 za wiki,Mwezi,Mwaka}
4.Zaburi 136:1-26{Sifa}
5.Mithali 1-31, Zaburi 1-150 {Soma Kila Siku Ukifuata Kalenda ya Mwezi}
6.Pakua Kutoka Kwa Mungu=Zaburi 104:4, Zab.23:1{Sitapungukiwa na… ‘Jaza’…
HUDUMA YA YESU KRISTO
#Isa.11:2{Roho 7 za Mungu}Bwana atakaa juu yake,Hekima,Ufahamu,Ushauri,Uweza,Maarifa,Kumcha Bwana
#Gal.5:22-23{Matunda 8 ya Roho}Upendo,Furaha,Amani,Uvumilivu,Utu Wema,Fadhili,Uaminifu,Upole,Kiasi
7. Ukiwa unasoma kama huwa una sinzia-sinzia, una piga miayo ama Uvivu-Yohana 14:26. Soma mara 3 kwa kurudia-rudia tena na tena kwa sauti.
8. Ukiwa una jiandaa na Usaili wa kazi ama umeitwa kujieleza-Luka 12:11-12
9. Ukihitaji Mafunuo na Mawazo Mapya- Waefeso 1:17-18
10.Ukihitaji Roho ya Ubora-Daniel 5:12, Dan 6:3
11.Roho ya Upendo/Huduma kwa Mteja, Soma vitabu vinne vya Injiri ya Yesu Kristo ambavyo ni Injini ya Mkristo.#Mathayo#Marko#Luka #Yohana
12.Kazi ya ADAM, Mwanzo 2:15. Simamia Yeremia 22:29, Isaya 1:19, Zab 24:1, Yohana 8:8, Isaya 3:10. Neno “Nchi” x2362=SUV; x2109=BHN
13.Kazi ya YESU KRISTO, Mathayo 1:21; Mt 6:33,Mt 11:5,12,Mk 10:29-30,Yn 15:16
14.SHUKRANI YA LISAA:Toba,Sifa,Shukrani=Kumkumbuka Mungu Kila Lisaa Zab.100:4,Zab.118:24,Zab.103:3, Zab.23:1,Gal.5:22-23,Isa.11:2,Ufu.5:12, Ufu.1:8. Kwa Nini? Kumb.8:18, Zab.119:164, Zab.55:17, Omb.2:19
MUHIMU: 
   Kila Mstari unao soma hasa ya Toba* Malizia “Kwa Maana            
  Fadhili zake ni za Milele-Katika Jina La Yesu Kristo wa Nazareti”.
    MAISHA SIYO BIASHARA YAKO NI BIASHARA YA MUNGU
    Yeremia 1:5, Mathayo 6:25-34, Isaya 54:13, Isaya 48:17. 
    Kwa Maelezo zaidi Piga simu au tuma SMS kwa namba  
    zifuatazo;
           Sir Bill Mushi Christ Jr. 0788 715 656/0786 989 867 
           Pilot Amanyisye  0782 050407/0755 746327 WhatsApp Kingdom* {Arusha}
Mr Excellent Emil 0763 048 173 {Shinyanga}
Bishop Baraka 0745 897 092/0685 433 249 {Nyamagana, Mwanza}
Pastor Martin 0767 546 679/0684 846 388 {Pasiansi, Mwanza}
Pastor Emmanuel 0758 439 190 {Dodoma}
Pastor Leonard 0719 890 175 {Geita, Mwanza}
Pastor J.Kalokola 0768 220 438 {Mianzini-Arusha}
Prophetess Mena 0763 219 702 {Arusha}
Pastor David 0784 246 424 {Mbeya Mjini} 
Mtumishi Gideon 0755 244 832{Moshi Mjini, Kilimanjaro}
Teacher/Pastor Elizabeth 0756 662 631 {Kijitonyama-Dar es Salaam}
Teacher/Mentor Ahazi Ngessy 0766 387 914/0688 960 066 {Kwa Mrombo-Arusha}
Mwalimu Michael 0788 618252/0745 196070/0654 202 464 WhatsApp {Ngusero-Arusha} 

The Future Business To Learn is
KINGDOM BUSINESS
                                                           ***YESU NI BWANA***

              2021-MWAKA WA AKILI INAYOPITA MIPAKA Kingdom Business Clubaship  leo Tumeingia Mwaka 2021, Kila Mwaka Tarehe Moja Ya Mwezi Wa ...