11th June, 2017.
THE LOVE OF GOD AND PEOPLE
(Mathayo 22:36-40)
KINGDOM BUSINESS (Mathayo 6:33)
TIME & BUSINESS COACH
Title: THE SPIRITUAL TIME ZONE/MAJIRA NA NYAKATI ZA KIROHO
#MARKO 14:32-42
Muda wa Kiroho nini?
Kupitia injili ya Luka, Yesu alipobatizwa,
alimiminiwa roho ya Mungu na kwamba Yesu alikuwa “amejaa roho takatifu.”
(Luka 3:21, 22; 4:1) Naye Yesu alikazia akilini mwa wafuasi wake umuhimu wa kuongozwa na roho mtakatifu wa Mungu, au ‘nguvu zake za utendaji.’ (Mwanzo 1:2; Luka 11:9-13)
Kwa nini hilo ni jambo la maana? Ni kwa sababu roho ya Mungu ina nguvu
ya kubadili akili ya mtu, ili ianze kufanana na akili ya Kristo aukomboe muda wake. (Waroma 12:1, 2)
Roho takatifu inatokeza ndani katika muda wa mtu huyu kupitia sifa kama vile “upendo, shangwe,
amani, ustahimilivu, fadhili, wema, imani, upole, kujizuia.” Sifa hizo,
ambazo Biblia inaziita “matunda ya roho,” zinaonyesha kwamba mtu fulani
ni mtu wa kiroho kikweli. (Wagalatia 5:22-23) Kwa ufupi, mtu aliye makini kiroho ni yule anayeongozwa na roho ya Mungu na akitambua majira na nyakati za kiroho.
Unapojua muda wako wa kiroho unakusaidia kukua kiroho, kama
hujui muda wako wa kiroho ni ngumu kukua kiroho na itakuwa ni ngumu pia
kumweshimu mtumishi wa Mungu yeyeto yule. Na ikitokea ukawa unamsikiliza
mafundisho atoayo itakuwa ni vigumu kupokea chochote kutoka kwa huyo mtumishi ‘jua
baba yako wa kiroho ni nani’. Majira na nyakati za kiroho zinakusaidia kumjua
baba yako wa kiroho mtoto wako wa kiroho, hili ni eneo ambalo linatesa watu
wengi kwa kutoweza kupokea kitu kutoka kwa Mungu au kupitia kwa mtumishi yeyote
yule.
Mwanadamu ana kua kimwili na kiroho(mwaka jana mwezi wa 12
tulifundisha Somo la MUDA. Tulisema umri
wako wa kimwili unakusababishia ufe mapema na umri wako wa kiroho
unakusababisha uishi muda mrefu. Umri wa kimwili unakusababsha utafute fedha na
umri wa kiroho unakusababisha utafute mambo ya kiroho(uumtafute Mungu) kwa
maana mwili ndiyo huchokao lakini roho yako ipo pale pale(Hebu ni wakumbushe
Kidogo tulicho fundisha…
MGAWANYO WA MUDA
Muda umegawanyika katika makundi makuu mawili. Katika
makundi haya ndipo watu wengi wamepakosea kwa maana wao wameuchukulia muda kwa
ujumla. Siku utakapo anza kuchulia muda kwa ujumla ndipo utakapo anza kuwa
MASKINI. Kwa wale wajanja kama sisi watu wa Kingdom Business “Matai” tunajua
muda umegawanyika katika makundi mawili kama ilivyo mitandao ya simu za mikononi
wanatoa vocha za airtime ya sauti(maongezi) na Data(internet-picha). Kila kitu
duniani jitahidi kukiangalia katika pande mbili. Maeneo ya muda ni kama
ifuatavyo
1. Physical Time / Muda wa Kimwili
2. Spiritual Time (Blessing)/ Muda wa Kiroho
PHYSICAL TIME
Ni muda ambao unatumia kwa mambo ya kimwili kwa mfano kula
chakula, kuangalia mpira, kwenda ofisini kufanya kazi, unafanya kazi mahali na saa
hiyo hiyo unalipwa, KULALA. Pamoja na hayo yote Namba moja kinacho UA leo muda
wa watu ni wengi Africa/Tanzania ni SIKANU au SMARTPHONE “Nashauri muda huu
usizidi 20% katika masaa yako 24” hata kama leo muda wako wa kimwili unatumia
80% badala ya 20% ANZA LEO KUJI” TUNE” MUDA WAKO WA KIMWILI UWE 20%. Kujizoesha
huku kunaweza kuchukua mpaka miaka 5!
SPIRITUAL TIME
Muda huu una umuhimu sana katika maisha ya kila mwanadam.
Thamani yake inatakiwa ifike 80% ya muda wako katika masaa 24 kwa siku.
Spiritual time ina vitu vifuatavyo;
Meditation-think-Kufikiri, Soma kitabu cha
Joshua 1:8
Prayers ( Maombi
Fasting/ Kufunga
Serving God/ Kumtumikia Mungu
Spiritual Time ndiyo muda unalipa zaidi kuliko kitu kingine
chochote duniani. Mungu anachotaka leo kutoka kwako siyo fedha ni MUDA WAKO TU.
Utoe muda wako kwa ajiri ya mambo ya Kiungu. Leo hii tunaona watu wengi
wanalipa kila kitu hakuna hata mtu anakuja anasema “hii nakulipia” kwa sababu
umetumia physical time sana kuliko spiritual time. Kwa maana nyingine ukiona
unalipa kila kitu ujue UNA KULA LAANA kwa sababu HUJATENGA MUDA WAKO KWA AJIRI
YA MAMBO YA KIROHO-SPIRITUAL TIME. Kwa Mfano Bishop David Oyedepo alitoa
muda mwingi kwa Mungu kujifunza na Mungu
akaingilia maisha yake.
Spiritual time unaipata pia kwenye kusoma vitabu, Huduma kwa
mteja, Kupitia maktaba yako nyumbani, Kusikiliza CD njema, Seminars, Maonyesho
ya biashara n.k. Spiritual time inakupa muda wa kufikiri kwa maana usi tafute
fedha ili ufanye jambo zuri hili ni kosa, Bali tafuta taarifa ili upate UTAJIRI
Mithali 8:10.
Hivyo basi ujue miaka yako ya kimwili isikudandanye ya kua
umekua kiroho. Mungu ni Roho haendi na mambo ya kimwili “Hutenda vitu vyake
kiroho” na sisi wanadamu ni roho aishiye
katika mwili huu na ikitokea umeangalia miaka yako ya kimwili ya kuwa ni mingi
ukadhani umekuwa kiroho si kweli jiangalie ni lini ulikata shauri na ukabatizwa
ukiwa na ufahamu(ukiwa mtu mzima) ndipo utakuwa ulianza kutemebea na Mungu
pamoja na Roho wake! Jiulize wewe umeanza lini kumjua Mungu kwa ufahamu na
kwenda kanisani? Una miaka mingapi umeanza kusoma maandiko matakatifu-Biblia?
ni lini ulinza kuwa serious na mambo ya kanisa, ulianza kuchukua notes za
mchungaji wako afundishapo-ukiandika, nymbani unasoma biblia, unaingia kwenye
kufikiri(maombi) na kufunga pamoja na mambo mengine mengi ya kiroho. Hivi ndiyo
muda wako wa kiroho ulivyoanza kuhesabiwa na si umri wako wa ugali. Umri wa nyama huwezi kufika mahali utaona
unaanza kuumwa, kuchoka na kuzeeka mwishoe kufa.
Kufanikiwa kwako si kutokana na umri ulio nao bali kulingana
na kiwango chako cha Imani ulichonacho. Ya kwamba una miaka mngapi
kiroho(utaanzia pale Yesu aliposema hawa watu lazima wazaliwe mara ya pili Yohana
3:3-8) yale maisha ya kabla hujazaliwa mara ya pili ni ujinga mtupu, Mungu
haesabu hata siku moja. Ukizaliwa mara ya pili unatakiwa usome maandiko
sana-Biblia, upunguze na uache dhambi, utembee na upendo kwa kila mtu na
usamehe pamoja na kusahau ndipo maisha yako ya kiroho yataimarika mara.
Umri wa kimwili unakusababsha utafute fedha na umri wa
kiroho unakusababisha utafute mambo ya kiroho(uumtafute Mungu) kama nilivyosema
hapo juu kwa maana mwili ndiyo huchokao bali roho yako ipo pale pale. Anza
kutembea na mwili wako wa wokovu(rohoni-mtu wa ndani), tafuta toba mara kwa
mara(Zaburi 51 yote, Zaburi 103:3), acha kuamini mambo ya kimwili anza
kuyaangalia Maneno ya Kristo.
Jifunze kujua majira na nyakati “Spiritual Time Zone” na
uanze kutembea nazo kuanzia sasa. Je unajua upo nyuma masaa mangapi kiroho?
Duniani kuna alama za masaa “World Time Zone”, alama hizi za masaa
zimetofautiana mpaka masaa 12 kwa mfano Tanzania na Uingereza tumetofautiana
masaa mawili (Sisi tupo mbele masaa mawili ya Uingereza), Tokyo- Japani wapo
masaa 6 mbele yetu, New York na sisi Tanzania tupo masaa 7 mbele ya New York.
Siku ukishajua upo masaa mangapi nyuma ndipo mahali maisha yako yanapo anzia.
Marko 14:32-42, jifunze kujua upi muda wako wa kiroho na upi
muda wako wa kimwili, utaona wale walio
amua ku’set muda wao mwingi katika mambo ya kimwili wengi wao ni wajinga
kabisa. Kwa mfano vijana wa umri wa miaka 20-25 wa sasa ambao hawana Nidhamu na
vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii tena vijana hawa hawa tafuti
maarifa stahiki “Maarifa ya Kiungu” tuwape muda wa miaka 40 tu ijayo yaani
wakifikisha miaka 60-65(tutakuwa na wazee wengi WAJINGA HUJAPATA KUONA).
Baba na mama yako walichokipanda ndicho una kivuna leo. Hata
hivyo pamoja na mateso ya watu wengi imechangiwa na vizazi vilivyo pita pamoja na wewe mwenyewe
kupitia namna ya matumizi yako ya muda. Badili mwelekeo wa maisha yako kuanzia
leo, kinacho kutesa leo kisije kikamtesa
kuanzia mtoto na watoto wa watoto wako Mithali 13:22.
Ukiachwa na muda nenda kwa spidi ili ufanikiwe, Mwanzo
13:14-15-Abraham alikuwa nyuma masaa 8. Utakavyo kuwa nyuma masaa mengi ndipo
wewe utaanza kuona mbali uendako! Usiwaze kifo “kama unatembea kimwili utawaza
vifo tu” tembea kiroho ujue kesho yako na jijengee ujisemee “lazima nifike
mbinguni hata kwa mtutu baada ya maisha haya”
Ili ufanikiwe lazima ucheze na kanuni ya Mungu, sasa
wakristo wengi tena wale hujiita walokole hawachezi na namba bali hucheza na
maneno tu”maombi”. Hufanya vitu kimwili na kusahau ya kuwa Mungu wetu ni wa Kiroho
tena yeye mwanadam huyu ni roho aishiye katika mwili(wewe).
Namba + Maneno=
Mafanikio
Katika ulimwengu wa kiroho kuna vitu vingi vinaongezeaka
endelea kupanda mbegu kwa kufanya kazi ya Adam (Mwanzo 2:15) na kazi ya Yesu (Mathayo
1:21; 6:33). Maneno hutengeneza hisia jifunze kuongea maneno mazuri kama vile
Yesu alivyosema katika Yohana 6:63. Hakuna kitu utapata maishani kama hujaanza
na hisia ya kitu hicho kama vile Yesu alivyo jifunua ‘alitoa ubunifu wake kwa
watu ili wamwelewe’ kulingana na maeneo tofauti tofauti kama alivyosema “Mimi
ni mdhabibu wa Kweli”-Yohana 15:1, “ Mimi ndiye ufufuo wa kweli na uzima-Yohana
11:25-27” n.k
HITIMISHO
Usilale na kuamka na
watu wajinga, ukienda mahali kama ofisini/kanisani/msikitini usikubali
kulala kama wao ulivyo wakuta bali wewe ukienda popote anza kwa kusafisha jina.
Umehamia nyumba mpya anza kufanya kitu ambacho zamani ulikuwa hukifanyi-acha
zile tabia za zamani ulizokuwa ukiishi nazo nyumba/ofisi ya zamani.
Unaswali/Maoni/Mapendekezo komenti hapo chini au Una
ushuhuda usisite kutuandikia Kupitia hapa au kwa rewiew section ya Facebook
(Tazama kwenye ukurasa huu
utaziona nyota hivi, ziweke upendazo baadae andika hapo-Asante.)

No comments:
Post a Comment