Yesu Mwana wa
Daudi, Hallelujah x3
JE! UNASHAUKU NA NIA YA KUFANYAKAZI? JE! UNAMAONO YA AJIRA?
“Kwa maana hata tulipokuwa pamoja nanyi, tuliwapa amri ili kwamba:
‘‘Mtu ye yote asiyetaka kufanya kazi, wala asile.’’ Kwa kuwa tunasikia kwamba
baadhi ya watu miongoni mwenu ni wavivu. Hawafanyi kazi bali hujishughulisha na
mambo ya wengine. Basi watu kama hao tunawaagiza na kuwaonya katika Jina la
Bwana Yesu Kristo wafanye kazi kwa utulivu na kujipatia mahitaji ya maisha yao
wao wenyewe.” 2 WATHESALONIKE 3:10-12
“Kwa maana viumbe vyote
vinangoja kwa shauku kudhihirishwa kwa watoto wa Mungu.” WARUMI 8:19
TAFUTA MAKAMPUNI BINAFSI MATATU, MASHIRIKA YA KIMATAIFA, NGO’S,
TAASISI ZA UMA, AU SEREKALINI.
“Ombeni nanyi mtapewa, tafuteni nanyi mtapata, bisheni nanyi
mtafunguliwa mlango. Kwa maana kila aombaye hupewa, naye atafutaye huona, naye
abishaye hufunguliwa mlango.” MATHAYO
7:7-8
‘ANDIKA BARUA ZA MAOMBI YA
KAZI SEHEMU TATU TOFAUTI, AMBATANISHA NA WASIFU WAKO “CV’S”.
“Nitasimama katika zamu yangu na kujiweka mwenyewe juu ya maboma,
Nitatazama nione atakaloniambia na ni
jibu gani nitakalotoa kuhusu lalamiko hili. Jibu La BWANA Kisha BWANA
akajibu: Andika ufunuo huu na ukaufanye wazi juu ya vibao ili mpiga mbiu
akimbie nao. Kwa kuwa ufunuo huu unasubiri wakati uliokubalika, unazungumzia
mambo ya mwisho na kamwe hautakosea. Iwapo utakawia, wewe usubiri, kwa hakika
utakuja na hautachelewa.”HABAKUKI 2:1-3.
CHUKUA HATI YA TABIA NJEMA KUTOKA POLISI.
Msidanganyike,
“Ushirika na watu wabaya huharibu tabia njema.” 1 WAKORINTHO 15:33
PELEKA MAOMBI YAKO YA AJIRA KWA MCHUNGAJI WAKO AU KIONGOZI WAKO WA IMANI AYABARIKI..
“Mungu
akawabariki na akawaambia, “Zaeni na mkaongezeke, mkaijaze tena dunia na
kuitiisha. Mkatawale samaki wa baharini, ndege wa angani na kila kiumbe hai
kiendacho juu ya ardhi.’’ MWANZO 1:28
“Mungu akaibariki
siku ya saba akaifanya takatifu, kwa sababu katika siku hiyo alipumzika kutoka
kazi zote za kuumba alizokuwa amefanya.” MWANZO
2:3
NENDA UKAFANYE KAZI KIMVULI KATIKA
VITUO VYA WATOTO YATIMA ,WAJANE, WAZEE, WATOTO WA MITAANI, KUTEMBELEA WAFUNGWA
KUWATIA MOYO, KWANDA HOSPITALINI KUOMBEA WAGONJWA, KUTUNZA MAZINGIRA, NA
KUHUBIRI INJILI, CHAGUA KAZI MOJA TU KATIKA HIZO HAPO JUU.
“Dini
iliyo safi, isiyo na uchafu, inayokubalika mbele za Mungu Baba yetu, ndiyo hii:
Kuwasaidia yatima na wajane katika dhiki zao na kujilinda usitiwe madoa na
dunia.” YAKOBO 1:27
“BWANA
Mungu akamchukua huyo mtu akamweka kwenye Bustani ya Edeni ailime na kuitunza” .MWANZO 2:15
“Kwa
maana nilikuwa na njaa mkanipa chakula, nilikuwa na kiu mkaninywesha, nilikuwa
mgeni mkanikaribisha, nilikuwa uchi mkanivika, nilikuwa mgonjwa mkanitunza,
nami nilikuwa kifungoni mkaja kunitembelea” MATHAYO 25:35-36
“Basi
wale wanafunzi kumi na mmoja wakaenda hadi Galilaya kwenye ule mlima ambao Yesu
alikuwa amewaagiza. Walipomwona, wakamwabudu, lakini baadhi yao wakaona shaka.
Yesu akawajia na kusema, “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Kwa sababu
hii, enendeni ulimwenguni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza
kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, nanyi wafundisheni kuyashika
mambo yote niliyowaamuru ninyi. Hakika Mimi niko pamoja nanyi sikuzote, hadi
mwisho wa nyakati.’’ Amen. MATHAYO 28:16-20
ANZA MAOMBI YA KUOMBEA WATU AMBAO
HAWANA KAZI WAPATE KAZI KWA KUSIMAMIA ANDIKO HILI
“Baada
ya Ayubu kuwaombea rafiki zake, BWANA akamfanikisha tena naye akampa mara mbili
kama yale aliyokuwa nayo hapo kabla.” AYUBU
42:10
INGIA KWENYE MAOMBI YA TOBA NA
REHEMA MARA SABA KWA SIKU
“Baba
Jehovah akusamehe dhambi zako zote na
kuponya magonjwa yako yote, kwa Damu ya Yesu kristo, Kwa maana fadhili zake
niza milele katika jina la Yesu kristo
wa Nazareth” ZABURI 103:3
“Ee Mungu, unihurumie, kwa
kadri ya upendo wako usiokoma kwa kadri
ya huruma wako usiokoma,yako kuu uyafute
makossa yangu yote kwa Damu ya Yesu kristo, Kwa maana fadhili zake niza milele katika jina la Yesu kristo wa Nazareth,” ZABURI 51:1
UTAKAPOKUWA
UNAJIANDAA KWENDA KATIKA USAILI SIMAMIA MAANDIKO HAYA
‘‘Watakapowapeleka katika masinagogi mbele ya watawala na wenye
mamlaka, msiwe na wasiwasi kuhusu namna mtakavyojitetea au mtakavyosema: Kwa
maana Roho Mtakatifu atawafundisha wakati uo huo mnachopaswa kusema.” LUKA 12:11-12
ANZA
KUMSHUKURU MUNGU KWA KUPATA AJIRA KILA BAADA YA DAKIKA SITINI LISAA LIMOJA.
MUNGU NI ALPHA NA OMEGA 59MINS-60MINS
“Shukuruni kwa kila jambo, kwa
maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu kwa ajili yenu katika Kristo Yesu.” 1 WATHESALONIKE 5:18
MASOMO HAYA YANATOLEWA BURE KATIKA OFISI ZETU ZA ARUSHA WASILIANA
NASI +255 788 71 56 56
SHARE, “WATUMIE NA WENGINE UJUMBE HUU
WAPATE KUJIFUNZE NA WAO”.
No comments:
Post a Comment