Thursday, October 1, 2020

             2021-MWAKA WA AKILI INAYOPITA MIPAKA

Kingdom Business Clubaship leo Tumeingia Mwaka 2021, Kila Mwaka Tarehe Moja Ya Mwezi Wa 10 Tuna Anza Mwaka MPYA. Tuna Kalenda Yetu Ambayo Tumeipa Majina Kuanzia Siku Mpaka Miaka Kupitia Majina Ambayo Sisi Tuna Fahamu Maana Yake. Tuliona Kutumia kalenda ya Kidunia Siyo Sahihi Na Wala Haina Maana. Hivyo Kalenda Yetu Ni kama ifuatavyo

                    KALENDA YA SIKU 7 ZA WIKI


1. JUMATATU= “Siku Ya Miujiza”

2. JUMANNE= “Siku Ya Hekima”

3. JUMATANO= “Siku Ya Nuru”

4. ALHAMISI= “Siku Ya Matumaini”

5. IJUMAA= “Siku Ya Kristo”

6. JUMAMOSI= “Siku Ya Imani”

7. JUMAPILI= “Siku Ya Ukarimu/Upendo”

                     KALENDA YA MIEZI 12

Majina ya Kalenda ya Mwezi ni kama Ifuatavyo:
1. JANUARY= "Maono"
2. FEBRUARY= "Kibali"
3. MARCH="Uchumi"
4. APRIL="Tai/Kasi/Spidi"
5. MAY="Nyota"
6. JUNE="Ufalme"
7. JULY="Uhuru"
8. AUGUST="Uaminifu"
9. SEPTEMBER="Mavuno"
10. OCTOBER="Kujipa Moyo"
11. NOVEMBER="Shuhuda"
12. DECEMBER="Neema"

                      MAJINA YA MWAKA

Tangu Huduma Hii Ilipoanza Rasmi Tarehe 1/10/2018 Miaka Miwili iliyopita Tumekuwa Na Majina Pamoja Na Maandiko Ya Kusimamia Mwaka Mzima Ni Kama Ifuatavyo:

2018-2019

KAULI MBIU
“The Love of the Truth and in Deed”/ “Upendo wa Kweli Katika Matendo”

NENO LA MWAKA;
Maneno ya Mungu ya Kusimamia yalikuwa “2 Wathesalonike 2:10” pamoja  na “1 Yohana 3:18”

2020

KAULI MBIU
“BE STRONG AND OF GOOD COURAGE”/ UWE HODARI NA MOYO WA USHUJAA

NENO LA MWAKA;
Neno la Mungu la Kusimamia linatoka Katika Kitabu cha Joshua 1:6 ambalo linasema Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana ni wewe utakayewarithisha watu hawa nchi hii niliyowaapia baba zao ya kwamba nitawapa.

                               2021

KAULI MBIU;

THE CROSS OVER MINDSET

            "AKILI INAYOVUKA MIPAKA"

Maelezo Kuhusu Kauli Mbiu hii
Mwaka 2021 Ni Mwaka wa Kuvuka Mipaka Bila Kuwa Na Passport, Vyeti, Kuvuka Mipaka Ya Umaskini, Mipaka Ya Kiuchumi, Ya Kifedha, Mipaka Ya Kiimani...Usikae Mahali Pamoja, Vuka Na Usiridhike Mahali Unapopitia.
Uwe Na Akili Inayovuka Mipaka, Uvuke Mipaka Ya Ugonjwa, Ya Dhambi... Ndiyo Maana Yesu Alipokuja Akasema Tuzaliwe Mara ya Pili-Kuzaliwa Mara Ya Pili Ni Kuvuka Ni Mipaka.

Mwaka Huu 2021 Tutakufundisha Jinsi Gani Ya Kutoka Kuishi Kwenye Nyumba Ya Kupangisha Mpaka Kwenye Nyumba yako Mwenyewe, Kutoka Kuishi Kwenye Nyumba Ya Udongo Mpaka Nyumba Ya Block, Kila Kitu lazima Uende Hatua Ili Uvuke Mipaka Hiyo, Lazima Mungu Akupe Roho Ya Kuvuka Mipaka. 
Kuna Watu Hawasafiri Kabisa Lakini Kwa Mfano Wazungu Wana Safiri Kwa Sababu Wana Roho ya Kuvuka Mipaka Kwenda Nchi Hadi Nchi-Hawaogopi Hata Kama Nchi Hiyo Ina Magonjwa au Vita. Vile Vile Kwa Mfano Tanzania Makabila yenye Roho ya Kuvuka Mipaka ni kama Wamasi na Wachagga! 

Usipo Safari Kuna Mengi Unakosa, Moja Ya Faida Ya Kuvuka Mipaka ni Akili Kuwa Mpya. Kitu Kinacho Safisha Akili Ya Mwanadamu ni KUSAFIRI Mara Kwa Mara Hata Basi Kwa Kutumia Mtandao "Virtue Travel".





NENO LA MWAKA;

MATHAYO 28:16-20
"Na wale wanafunzi kumi na mmoja wakaenda Galilaya mpaka mlima ule aliowaagiza Yesu. Nao walipomwona, walimsujudia; lakini baadhi yao waliona shaka. Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari."

  • "MBINGUNI NA DUNIANI" NI KUVUKA MIPAKA
  • Kuwafanya Watu Kuwa WANAFUNZI WA YESU Ni Kuvuka Mipaka
        MWAKA 2021 NA UWE MWAKA WAKO WA KUVUKA MIPAKA KATIKA MAENEO YOTE YA MAISHA YAKO...

SALAMU YA MWAKA 2021

MWAKA 2021
Caller: YAI FOR CHRIST 2021                                                                                                                
Response: 2021
Caller: YAI FOR CHRIST


Kwa Mawasiliano Zaidi
Mwalimu Bill Mushi , 0788 715656 au 0677 715656
Mtumishi Leonard Kapala, 0769 900401 WhatsApp Group}
Pilot Amanayisye Urassa, 0782 050407 {WhatsApp Group}
                      
                               YESU NI BWANA


1 comment:

  1. Mungu ibariki kingdom business na uongozi wake..wabariki wanafunzi na walimu wake wabariki wote wanaobarikiwa na huduma hii kama mimi na wengine wote......

    ReplyDelete

              2021-MWAKA WA AKILI INAYOPITA MIPAKA Kingdom Business Clubaship  leo Tumeingia Mwaka 2021, Kila Mwaka Tarehe Moja Ya Mwezi Wa ...