Habari za leo Mwana wa Mungu, Kila Tarehe 1,ya mwezi wa 10, Huduma hii ya KINGDOM BUSINESS CLUBSHIP Duniani huanza na Mwaka Mpya, KWA HIVYO KILA TAREHE 1 MWEZI WA 10 NDIYO MWAKA MPYA WETU. Kwa kusema hivyo basi tulianza mwaka MPYA-2020 tarehe 1 mwezi huu. Tunapoanza mwaka huduma hutoa Neno Na Kauli mbiu ama kwa lugha ingine NENO LA KUTEMBEA NALO MWAKA MZIMA. Kwa mfano tulianza mwaka jana 2018-2019 mwezi wa 10 tarehe 1 na:
MWAKA 2019 Tulikuwa na Neno Linalosema
KAULI MBIU;
Caller: YAI FOR CHRIST 2019
Response: 2019
Caller: YAI FOR CHRIST
NENO LA MWAKA MZIMA LILIKUWA;
“The Love of the Truth and in Deed”/ “Upendo wa Kweli Katika Matendo”
Maneno ya Mungu ya Kusimamia yalikuwa “2 Wathesalonike 2:10” pamoja na “1 Yohana 3:18”
Oktober 1 tuliingia mwaka mpya 2020, Na Neno la mwaka huu linasema
“BE STRONG AND OF GOOD COURAGE”/ “UWE HODARI NA MOYO WA USHUJAA”
Pia tuliondoka kwenye kutumia kalenda ya kidunia kwa kuanza kuzipa majina SIKU, MWEZI NA MWAKA tangia mwisho wa mwaka jana. Mwezi huu wa 10 ninyi mmeuzoea kuita OCTOBER ila sisi tumeupa jina la THE COURAGE yaani UJASIRI au USHUJAA hivyo namba 10 kwetu sisi ni Ushujaa kwako Wewe je unauhitaje? Bado miezi miwili tukamishe Kalenda yetu yam waka mzima.
MWAKA 2020 Neno linasema;
KAULI MBIU:
Caller: YAI FOR CHRIST 2020
Response: 2020
Caller: YAI FOR CHRIST
NENO LA MWAKA;
“BE STRONG AND OF GOOD COURAGE”/ UWE HODARI NA MOYO WA USHUJAA”
Neno la Mungu la Kusimamia linatoka Katika Kitabu cha Joshua 1:6 ambalo linasema “Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana ni wewe utakayewarithisha watu hawa nchi hii niliyowaapia baba zao ya kwamba nitawapa.”
Caller(Mtu akikwambia): 2020
Response(Unajibu): “Be Strong and of Good Courage” au "Uwe Hodari na Moyo wa Ushujaa"
Mungu alimwambia Yoshua “Uwe Hodari na moyo wa ushujaa”- Usiogope. Mungu alirudia kumwambia Yoshua mara 7 awe Hodari na moyo wa Ushujaa. Kukiwa kuna moyo mzuri wa ushujaa(hutoka kwa Mungu) ujue pia kuna MOYO MBAYA WA USHUJAA PIA(yaani namna ya kupenda fedha/Mali/dunia hii). Kuna mfano wa watu wa aina mbili hapa ambao wote walikuwa ni MAJUSHAA. Rais Mtaafu wa Afrika ya Kusini NELSON MANDELA alikuwa na MOYO MZURI WA USHUJAA lakini tuna Mwingine Dikteta Adolph Hitler alikuwa na MOYO MBAYA WA USHUJAA.
Swali kwako, Je wewe una moyo wa aina gani katika Maisha unayopitia hivi leo? Ni kitu gani kina kuogopesha ya kwamba watu au jamii ikijua utafadhaika sana? Ni wapi Umekosa Ujasili au umekwama? TUANDIKIE SMS AU COMMENT HAPO CHINI
Kwa Mawasiliano Zaidi
Mwalimu Bill Mushi , 0788 715656 au 0677 715656
Mtumishi Leonard, 0756 877161 au 0621 133985
Pilot Ami, 0782 050407{WhatsApp Group}
YESU NI BWANA


No comments:
Post a Comment