Niite Amanyisye (Kwa marafiki zangu huniita Pilot Ami au Mwana wa Isakari 1 Nya 12:32), ni Mfuasi wa Kristo, mmoja wa wanafunzi wa Bwana Bill Mushi 'Mwalimu' (Kingdom Business), nasimamia Kitengo cha Kingdom Media ama IT Program Manager.
Kingdom Business ni Mfumo mpya wa biashara unao kufanya uanze biashara pasipo kuwa na mtaji wala kukopa mahala popote pale, kwa wale wanohitaji ajira unapata kazi pasipo kuwa na cheti cha shule au chuo! Biashara hii ya kifalme "Kingdom Business" hatupendelei dini/huduma/kanisa lolote lile kazi yetu kubwa ni Kufanya kazi ya Mungu (Kazi ya Adam-Mwanzo 2:15, Kazi ya Yesu Kristo Mathayo 1:21; 6:33) na kuwapeleka watu kwa Kristo "wawe wanafunzi wa Yesu Kristo na si Washarika-Mathayo 28:19. Tuna tamani watu wote wamtumikie Mungu katika maisha yao yote "Love of God, People and Soul". Chuo hiki cha mafunzo, ni taasisi ya kifedha ambayo tunawafundisha watu namna ya kufanya biashara iliyo halali ikiunganishwa na neno la Mungu "Kufanya Biashara na Mbingu" kwa Lugha rahisi kabisa ni Ujasilimali jumlisha Biblia.
Tuna tumia Neno kuu kutoka Mathayo 6:33 ambalo linasema "Bali utafuteni
Kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa."
Tunatumia sana vitabu viine vya injiri ya Yesu Kristo ambavyo ni Mathayo, Marko, Luka na Yohana lakini kwa sababu Hekima ni ulinzi na utajiri tunasoma kitabu cha Mithali kila siku. Unaweza kujiuliza kwa nini tunatumia vitabu vya Injiri sana? kwa sabau ya UPENDO "Yesu Kristo ni upendo, alipokuwa duniani hakumhukumu mtu au kulalamika, alisamehe na kufuta dhambi "The love of God and People".
Kwa
sasa tupo chini ya kanisa la Winners' Chapel International-Arusha lipo
Kaloleni karibu na round about ya Florida kama unaelekea mianzini, nyuma
ya kituo cha mafuta cha Bambras. Siku siyo nyingi Kingdom Business ita
sajiliwa na kuwa na ofisi zake, vipeperushi, business
card n.k . Ikumbukwe tunatumia tu
jukwaa/ukimbi wa kanisa la Winners' Chapel International-Arusha kwa muda Fulani
MITAANI: Tupo mitaani arusha kila siku kuanzia Saa 6 mchana mpaka saa 2 usiku tangu mwezi wa 9 mwaka 2015 na tunaenda mpaka septemba,2018. Kwa wale wanao ishi Arusha na maeneo ya jirani kama ulishawahi kumwona Mwalimu akifundisha na ubao mweupe,spika, na kausafiri ndiyo huduma hii. Siku ya Jumapili pekee tunakuwa pale Kanisa la Winners' Chapel International-Arusha kuanzia saa 10-12 jioni na siku ya Jumatatu kuanzia saa 6 mchana mpaka saa 8 mchana-madarasa haya ni kama madarasa mengine hakuna kiingilio wala sadaka,watu wa dini zote wanaruhusiwa.
GHARAMA: "Muda wako tu" ,Mafunzo haya ni bure kabisa kwa watu wa dini zote. Ukija kwenye madarasa yetu tunakupa mpaka peni na karatasi ya kuandikia ili ujue kwamba tumedhamilia kutoa ujinga vichwani mwa watu! Luka 4:18
USHAURI NI BURE: Kama ungependa kukutana na Bwana Bill Mushi au sisi wanafunzi wake tupo na unaweza kuongea ana kwa ana (siku ya jumapili na jumatatu) ukieleza tatizo lako labda la kazini kwako, biashara na hata mambo mengine ya kimaisha ikiwemo ndoa na uchumba! Hakuna appointment wala ghalama ya kumuona yeyote yule. Ukipata nafasi fika ujifunze mitaani jijini Arusha (Tupo stand ya Namanga kila siku kasoro siku ya jumapili tu kuanzia saa 5:45 jioni mpaka saa 2 usiku) au Kanisani siku ya Jumapili(jioni) na Jumatatu(mchana) ama ukishindwa utapata mafunzo haya (audio na maandishi) hapa ama kupitia mitandao ya kijamii.
Tupigie kwa Ushauri/WhatsApp's Group 0782-050407/0763-048173
Pendezwa na ukurasa wetu wa Facebook
Tufuate nasi tutakufuata katika Instagram
The Future Business To Learn is Kingdom Business
AMANYISYE S.J.URASSA
IT Project Manager.
Jesus is Lord!
No comments:
Post a Comment