Yesu Mwana Wa
Daudi, Hallelujah x3
FANYA
KAZI KWA MUDA SIYO KWA MIKONO
2 WAKORINTHO 5;7
Tajirika Na Muda - Tumia Muda
Kibiashara
Waefeso 5:15-17
Kufanya Kazi Kwa
Muda Na Siyo Kwa Mikono Maana Yake Kufanya Kazi Kwa Kutumia Muda Wako Mwenyewe Wa Masaa 24Hrs Na Kutumia
Muda Wa Watu Wengine. Huwezi Kutajirika
Kwa Masaa Yako 24hrs Tu Bali Kwa Kutumia Muda Wa Watu Wengine.
Ili Uwe Na Muda
Zaidi Ya Masaa 24Hrs Chukua Masaa 10Hrs Ya Watu Wengine Kumi(10x10=100)
Jumlisha Na Ya Kwako 24Hrs Utakuwa Na Masaa 124Hrs Kwa Siku, Siyo Masaa 24Hrs Kama Watu Wa Kawaida.
UTAJIRI UPO KWENYE MUDA SIYO KWENYE PESA.
‘’Foolish people
use heart to think, But Smart people use brain to think’’.
Tasfiri Ya Kazi
Ya Muda Ni Kufikiri, Kutengeneza Ajira, Wazo La Biashara Na Kutafuta Taarifa
Kama Vile Unavyosoma Taarifa Hizi.
Wazungu Wanapigana
Na Vita Vya Ujinga, Waafrika Wengi Sana Wanapigana Na Vita Vya Umaskini’. Ukisikia Mtu Ana Kwambia
Yule Bwana Ni Mzungu Kwasababu Anatumia Muda Vizuri Anachokisema Ndicho
Anachokifanya, Akikuambia Ni Mswahili Basi Kuna Changamoto Hapo. UKISEMA JAPAN
UNASEMA MUDA UKISEMA AFRIKA UNASEMA PESA.
Watu Wote
Waliofanikiwa Duniani WALIFANYA KAZI ZA MUDA NA SIYO ZA MIKONO! Kuna Aina Mbili
Za Kazi Hapa Duniani; Kazi Za Muda Zinahitaji Kufikiri
Sana. Kuajiriwa Siyo Kitu Kibaya Bali
Ujue Umenyanganywa Uwezo Wa Kufikiri Asilimia 98%.
- AKILI KAZI –KUJIAJIRI- Mungu Anabariki
Kazi Ya Akili Yako. 1 KOR 15:34
- MKONO KAZI-KUAJIRIWA-Mungu Anabariki Kazi Ya Mkono Wako. KUMB. 28:12
Kazi Zote
Zinazofanywa Na Akili Zinafanywa Kwa Muda Na Zile Zinazofanywa Kwa Mikono
Zinafanya Kwa Nguvu . Kwa Kuwa Kazi Zote Za Akili Hazi Hitaji Nguvu Wala Vyeti
Vya Chuo Bali Zina Hitaji Muda Tu. Ajira
Unayotafuta Leo Ni Ya Aina Gani? Je, Ni Ya Kutumia Muda Au Kutumia Mikono?
Kazi Ya
Akili Unaanzisha Mwenyewe Kwa Kufiri Kwa
Kina.Na Hauhitaji Vyeti Ni Ubunifu Tu, Katika Huduma Hii Ya Kingdom Business
Clubship Tuna Kufundisha Matumizi Ya Muda Wako Katika Kazi Zote Mbili Kazi Ya
Akili Na Kazi Ya Mikono. Kazi Ya Akili Ni Kujiajiri Mwenyewe, Na Kazi Ya Mikono
Ni Kuajiriwa. Utakapo Anza Kufikiri Kila Kitu Mwenywe Na Kutumia Akili Yako
Asilimia Mia Moja.
Meneja Wa Benki Anatumia
Akili Yake Asilimia Mbili Tu Mama Anayechoma
Mahindi Anatumia Akili Yake Asilimia Mia Moja, Kwa Kutafuta Masoko, Kujali
Wateja, Matangazo, Nk. Mama Huyu Anafanya Hivi Vyote Mwenyewe. Na Yule Meneja
Wa Benki Amerahisishiwa Vitu Kwani Kuna “System” Mfumo Wa Kila Kitu Anakikuta Kazini.
AKILI
KAZI NA MKONO KAZI Ni Kufikiri Kwa Matendo, Yaani Unafikiri Huku
Unafanya Hii Ndiyo Njia Peke Yake Inaweza Kumtoa Mtu Katika Umaskini. Muda Unapewa
Na Mungu Pesa Unatafuta Mwenyewe, Mungu Anakupa Unachokiitaji, Hakupi Unacho
Kitaka. Unahitaji Muda Kutafuta Unacho Kitaka. 1 WAFALME 3:5, MITHALI
30:7-9
MWISHO
WA SEHEMU YA PILI
SEHEMU
HII NI YA MAANDIKIKO MATAKATIFU:
“kwa maana twaenenda kwa imani wala si
kwa kuona.” NEN 2 WAKORINTHO 5:7
“Kwa hiyo iweni waangalifu jinsi
mnavyoenenda, si kama watu wasio na hekima, bali kama wenye hekima, 16mkiukomboa
wakati, kwa sababu nyakati hizi ni za uovu. Kwa hiyo msiwe wajinga, bali mpate
kujua nini yaliyo mapenzi ya Bwana.” NEN WAEFESO 5:15-17
“Zindukeni mwe na akili kama iwapasavyo,
msitende dhambi tena, kwa maana watu wengine hawamjui Mungu. Nasema mambo haya
ili mwone aibu.” NEN 1 WAKORINTHO15:34
“BWANA atafungua mbingu, ghala zake za
baraka, kukupa mvua kwa majira yake na kubariki kazi zako zote za mkono Wako.
Utakopesha mataifa mengi lakini hutakopa kwa ye yote.” NEN KUMBUKUMBU LA TORATI
28:12
“BWANA akamtokea Solomoni huko Gibeoni wakati
wa usiku katika ndoto, naye Mungu akasema, ‘‘Omba lo lote utakalo nikupe.’’ NEN 1 WAFALME 3:5
“Ninakuomba vitu viwili, Ee
BWANA, usininyime kabla sijafa: Uutenge mbali nami udanganyifu na uongo,
usinipe umaskini wala utajiri, bali unipe chakula cha kunitosha kila siku.
Nisije nikawa na vingi vya kuzidi nikakukana na kusema, “BWANA ni nani?’’ Au
nisije nikawa maskini nikaiba, nami nikaliaibisha jina la Mungu wangu” NEN MITHALI
30:7-9
MASOMO HAYA YANATOLEWA BURE KATIKA OFISI ZETU ZA ARUSHA WASILIANA
NASI +255 788 71 56 56
SHARE, “WATUMIE NA WENGINE UJUMBE HUU
WAPATE KUJIFUNZE NA WAO”.

No comments:
Post a Comment