Monday, October 21, 2019

FORMULA YA UJASIRIAMALI, MAISHA, BIASHARA NA HUDUMA (FORMULA 0-9)


Salamu
Yesu Mwana Wa Daudi, Hallelujah X3

FORMULA YA UJASIRIAMALI, MAISHA, BIASHARA NA HUDUMA (FORMULA 0-9)
 ANDIKO KUU: Mithali 3:13-20 “19-20”
"Kwa hekima BWANA aliiweka misingi ya nchi;
Kwa akili zake akazifanya mbingu imara;
Kwa maarifa yake vilindi viligawanyika;
Na mawingu yadondoza umande"

MAANDIKO MENGINE: Methali 2:1-22, 4:7, 23:23. Yakobo 1:5, 3:15-17, Isaya 11:2


Watu Wote Wajanja Duniani Walifudishwa Kuhesabu Kuanzia 0-9(Watu Hawa Walikuja Duniani Kama MBEGU "Walitengenezwa Kama Mbegu"-LUKA 8:11). Watu Wa Aina Ya Pili Walikuja Duniani Kama MKATE Ambao Walifundishwa Kuhesabu 0-100(Mashuleni, Vyuoni, Walitengenezwa Pia!!!

Ukiangalia Vifaa Vyote Duniani Vya Mashine “Analog Or Digital Machines” Zimewekwa Namba 0-9, Angalia Simu Yako Sasa Hivi Ina Namba Ngapi?= 0-9

Kikokotozi Cha Mahesabu Yote Duniani “Calculator” Hupigwa Kwa Namba Hizi Tu 0-9. Hivyo Basi Jifunze Leo Kwa Mtiririko Huu (Ufuatao) NA HUTAKIWI KURUKA HATA NAMBA MOJA(Utapata Ajali). Unatakiwa Siku Zote Uanze Na "0" KWENDA "9"...Hata Gari Huanza Na Spidi 0.

FORMULA 0-9
0-LOVE/UPENDO=1 Kor 13:8, Luka 10:27, 1 Yohana 3:18, Wim 8:6, Yohan 3:16, Gal 5:22-23
1-TIME/MUDA= Mwa 1:1, Efe 5:16, Kol 4:5, Yn 5:17, Mhu 3:1
2-INFORMATION/TAARIFA=Isa 34:16, Yoh 1:8, Efe 1:17-18
3-KNOWLEDGE/MAARIFA=Yer 3:15, Hos 4:6, Isa 5:13
4-UNDERSTANDING/UFAHAMU=Mit 3:13, Mit 13:15
5-FAITH/IMANI= Rum 10:17, Ebr 11:1-6, Gal 5:6
6-WISDOM/HEKIMA= Isa 11:2, Yak 3:17, Yak 1:5, Mit 24:3-6, Mit 3:19-20, 1Kor 3:6-7
7-PEOPLE/WATU= Mt 4:19, Yn 21:15-17, Mit 11:30, 2 Pet 3:9
8- CASH/FEDHA A.K.A MONEY/PESA=Mt 6:24, 1Tim 6:10, Efe 5:5, Mit 23:4, Mit 28:22
9-THINGS/VITU"UTAJIRI"= Mt 6:33, Kut 23:25-26, Ayu 36:11, Isa 3:10, Yn 15:16, 2 Nya 9:1-12, Mwa 13:2, Mwa 24:35, Zab 112:3, Mit 10:22

UFAFANUZI WA FORMUAL 0-9
Chochote Unachokita Duniani Unaweza Kukipata Hata Kama Ni KIPAWA AU SKILLS!!!

TALENT/GIFT “KIPAWA”
Kipawa (KUJIFUNZA KUPITIA MAZOEZI/PRACTICAL) Ni ZAWADI Kutoka Kwa MUNGU. Lakini Mimi Nasema Ukitumia “0-9 Formula” Kwenye Jambo Fulani au Lolote Lile Pia Ukitafuta KIPAWA CHOCHOTE KILE LAZIMA UTAKIPATA YAANI MUNGU ATAKIWEKA KIPAWA HICHO MIKONI MWAKO-KItabu Cha Kutoka 31:1-5 (Mtu Huyu Anaenenda Kwa Imani “Mind Sight”

SKILLS “UJUZI”
Ujuzi(Mimi nauita KUJIFUNZA KUPITIA THEORY-Makaratasi tu) Una Patikana Kupitia Shule/Chuo. Mtu Anayehitaji UJUZI Ni Kwa Ajili Ya Kutafuta Ajira Aajiliwe... Yaani Apate Cheti, Mtu Huyu anaenenda kwa Kuona “Eye Sight”.

MCHANGANUO WA 0-9
0=UPENDO, Ukikipenda Kitu Chochote Duniani UKIKIPENDA Utakipa 1=MUDA, {Kazi Ya Muda Ni Kufikiri, Kutengeneza Mawazo Mapya Na Kutafuta Taarifa} Kwa Hivyo Ukitoa tu Muda Wako Kile Kitu Kitakuletea 2=TAARIFA, Taarifa Zikizidi Zitakuletea 3=MAARIFA, Maarifa Yakizidi Kwa Wingi Yatakuletea 4=UFAHAMU {Watu Wengi Sana Hufanya Vitu Pasipo UFAHAMU, Ukiona Kwenye Biblia Pameandikwa UFAHAMU Maana Yake ni AKILI, -Akili ya Mtu Haikui Kwa Umri INAKUWA KWA TAARIFA UNAZOPATA.
KWA HIVYO 4=UFAHAMU Ukizidi/Ukiongezeka Ndipo 5=IMANI Inaingia{Soma Maandiko Pale Juu KUHUSU IAMANI}. ILI IMANI YAKO IKAMILIKE LAZIMA IWE NA VITU VITATU
a) ZAO LA IMANI Mf. Rozari ya Katoriki, MAJI YA HUDUMA MBALIMBALI, STICKERS ZA HUDUMA n.k
b) HUDUMA YA IMANI Mfano Kutembelea Na Kusaidia  YATIMA “KWENDA KUFANYANYA KAZI YA YAI”
c) NENO LA IMANI “ Your KEYWORD”, Neno La Kusimamia

Imani Yako Ikizidi Ndipo 6=HEKIMA inazaliwa Sasa. Hekima ni nini? HEKIMA NI KITU CHA MWISHO KABISA. Hekima Inaonekana Kwa Wanadamu Kupitia Vitu Wanavyo Tengeneza Kwa Magfano Utaona Mtu Anatengeneza Kitu Kwa Ubora Wa Hali Ya Juu Ambapo Hakuna Mtu Mwingine Duniani Anacho(KIPAWA) Ana Mtumia SANA MUNGU wa OMEGA “FINISHING GOD” {Ufu 1:8}

BADO TUPO KWENYE 6=HEKIMA, Mfalme Sulemani Alianza na 0=UPENDO "Sulemani naye akampenda Mungu"= 1 Fal 3:3, Sulemani Alilipa DENI LA Upendo kwa Mungu  KWANZA na Mungu akampa HEKIMA(Hekima ya Uongozi)
HEKIMA ikizidi Unaipeleka kwa 7=WATU, Watu Watakupa 8=FEDHA. Kuna tofauti Kati FEDHA/CASH na MONEY/PESA. Pesa ni ROHO na Fedha ni FEDHA TASLIM Tunaziona Kupitia Noti Na Safaru. FEDHA ikija sasa wewe unanunua 9=VITU, UTAJIRI unaingia.

Jiulize Unafuata Hivi?
Sasa Watu Wengi Sana Huanza KWA KASI Kutafuta Namba 8=FEDHA Moja Kwa Moja Wakati Hawana Vitu Vya Mwanzoni UPENDO-MUDA-TAARIFA-MAARIFA-UFAHAMU-IMANI-HEKIMA-WATU Ndio ije FEDHA. Fedha ndiyo BIASHARA YA KWANZA Kuifanya na vile vile Ndio BIASHARA YA MWISHO KUIFANYA

Utakuta Ukimpigia mtu Simu Kwa Mara Ya Kwanza au Ukakosea Kutuma SMS Utakuta anakutumia SMS au Ana Kupigia Simu anakuuliza "WEWE NANI" BADALA Alitakiwa Akuulize, “Habari za saa Hizi, Samahani Naona Imekuja tu Namba bila Jina, Napenda Kukufahamu Sijui Mwezangu Nani?” BADALA YAKE NANI WEWE Unajua Maana Yake Nini Msemo Huu?
1.ANA HASIRA, AMEUDHIWA HUKO ANA KULAUMU WEWE
2."MIMI SIPENDI WATU" Maana yake USINISUMBUESUMBUE,
3.TABIA YANGU SI NJEMA NAPENDA KUKAA MWENYEWE Wakati Huku Ana Sema Biashara Ngumu Na huku Hapendi Watu. Jifunze KUZUNGUMZA Pamoja Na KUANDIKA LUGHA NZURI KWENYE SIMU.

HITIMISHO
“Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki.”  SUV YAKOBO 3:17 

SHARE HII, “WATUMIE NA WENGINE UJUMBE HUU WAPATE KUJIFUNZE NA WAO”.

No comments:

Post a Comment

              2021-MWAKA WA AKILI INAYOPITA MIPAKA Kingdom Business Clubaship  leo Tumeingia Mwaka 2021, Kila Mwaka Tarehe Moja Ya Mwezi Wa ...