Saturday, October 26, 2019

BADILISHA MUDA KUWA AJIRA NA GEUZA AKILI KUWA HEKIMA


JINSI YA KUTENGENEZA AJIRA SEHEMU YA TATU
Salamu!
Yesu Mwana wa Daudi, Hallelujah x3

"BADILISHA MUDA KUWA AJIRA NA GEUZA AKILI KUWA HEKIMA"
UFUNUO WA YOHANA 11:6, MITHALI 3:5, ZABURI 111:10
WARUMI 12:2, 1WAKORINTHO 15:34

Tajirika Na Muda –Tumia Muda Kibiashara
Waefeso 5:15-17, Wakolosai 4:5


Mungu amempa Mwanadamu uwezo mkubwa sana. Mwanadamu anaweza kugeuza Muda kuwa chochote anachotaka kwa kufikiri kwa kina. ‘’Hapo Mwanzo Mungu aliziumba Mbingu na Nchi’’ -Mwanzo ni Muda- ‘’KUTAFAKARI’’
ZABURI1:1-3 JOSHUA 1:8 UFUNUO 11:6

Mwanadamu anaweza kugeuza akili kuwa pesa. Mungu alimpa Sulemani Hekima akaigeuza akili kuwa Utajiri.
Kugeuza akili kuwa Hekima ni kubadili akili kuwa vitu. Mawazo ni vitu Geuza Mawazo yako kuwa Sayansi ,Tekinolojia Ufundi, Vitabu, Semina, Sinema na DVD;s, CD’s nk.

Hekima ni kitu cha mwisho, ukiona Magari ya aina ya Toyota ni Hekima ya MJAPANI – ‘’Japanese Wisdom’’.

Katika Roho Saba za Mungu, Nne zinahusiana na Hekima. Roho ya ufahamu ni Hekima, Roho ya Ushauri ni Hekima, Roho ya Maarifa ni Hekima na Roho ya Hekima ni Hekima. Ukigeuza Akili kuwa Hekima huwezi kushindwa mahali popote Duniani na Mbinguni-ISAYA11:2

Ukitengeneza ajira kivuli utapata faida kivuli na faida kivuli inatengeneza faida hasili. Ajira kivuli ni kazi za Kijamii, Ukipanda Mbegu ya Kazi utavuna Matunda ya Kazi. Ajira ni kama nyumba huwezi kujenga nyumba bila kuwa na Ramani ya jengo. Ramani ni nyumba kivuli.

Anza kidogo kidogo mwenyewe na Muda wako wa masaa 24Hrs mpaka ufikie kiwango cha Kugeuza Muda kuwa Ajira. Wewe unafikiri wengine wanafanya kazi.

Ajira kivuli ndiyo jibu la kila Mtanzania na Dunia kwa ujumla. Ramani ya Ajira ni kazi za kijamii-MATHAYO 6:33

Ajira kivuli ni Kazi ya Yesu, Kazi ya Adamu na Kazi ya Injili.
Kazi ya Yesu ni kusaidia Yatima,Wajane, Wafungwa, Wagonjwa, Watoto wa Mitaani,Walemavu, Wazee na Wasio jiweza.

Kazi ya Adamu ni Kutunza Mazingira, Wanyama, Misitu na Vyanzo vya Maji.

Kazi ya Injili Kufundisha Habari Njema.

KUMBUKA KWA MUNGU HAKUNA KUJITOLEA ANALIPA KILA BAADA YA DAKIKA SITINI. "60MINS"-LISAA LIMOJA’, UNAMCHAJI MUNGU KWA KILA LISAA LIMOJA KIWANGO UNACHOTAKA KULINGANA NA UZITO WA KAZI UTAKAYO FANYA-MATHAYO 20:1-16

Kama unahitaji kazi lazima utembee kwenye agano la kazi upande Mbegu ya kazi uipe muda utavuna matunda ya kazi yako. Kila kitu unachokiona Duniani kina Mbegu, nikikupa Tsh 1000 Sasa hivi kuna mbegu ndani yake asilimia moja ambayo ni Tsh Shilling kumi-MWANZO 8:22

Ukiona Wazungu wana kuja Afrika kufanya kazi za kijamii kama kwenye Vituo vya Watoto Yatima, Mashule, Hospitali, Kutunza Mazingira, NGO’s mbalimbali wamekuja kupanda mbegu ya kazi. Mungu anataka umuonyeshe kazi ya mfano ili aweze kukutengenezea Ajira.

Kazi ya Muda ni Kufikiri, Kutengeneza Ajira, Wazo la Biashara na Kutafuta Taarifa. Kazi ya Muda siyo kutafuta pesa, Kazi ya pesa ni kuukomboa Muda wako. Kwa mfano Safari ya kutoka Arusha mpaka Dar ess salaam kwa Basi ni masaa kumi , ukisafiri kwa Ndege ni lisaa limoja kwahiyo ukipanda Ndege utakuwa umekomboa masaa tisa, Hiyo ndiyo kazi ya pesa, WAEFESO 5:15-17, WAKOLOSAI 4:5

Mimi nimebadili Muda wangu kuwa ajira na nimegeuza Akili yangu kuwa Pesa. Kila mtu anaweza kufanya kama nilivyo fanya mimi, 1 WAKORINTHO 15:34

Ajira yako ipo ndani ya Muda wako na pesa zako zipo ndani ya akili yako kila mtu anao Muda wa masaa 24hrs na kila mtu anazo akili. Akili haitengenezi Pesa mpaka ibadilike kuwa Hekima. Sulemani alitatua matatizo ya watu kwa kutumia Hekima. Mfalme Sulemani hakutatua Matatizo kwa kutumia Pesa kama Dunia ya Leo walio wengi wafanyavyo. Utakapotatua tatizo la mtu kwa muda wako na akili yako atakulipa.

Akili ni rafiki mkubwa wa muda mahali akili yako itakapo kwenda ndiko muda wako utakapo kwenda, kitakachomea kwenye Ubongo ndicho kitakachomea kwenye moyo wako, MITHALI 23:7 MATHAYO 6:19-21

Kazi ya Akili ni kuuza Muda kwa Faida, Akili ikishindwa kuuza Muda mtu huyo basi anaitwa Maskini. Mungu na wanadamu wote wananunua Muda. Mungu analipa vizuri kuliko wanadamu. Mungu ni mwaminifu sana na analipa wakati huo huo ukimaliza kazi yake.

Watu wengi hawajui mfumo wa Mungu anaotumia kuwalipia watu wanao mtumikia katika ufalme wake. Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika Roho na kweli. Watu wanajua mifumo ya kimwli tu hawajui mifumi ya kiroho. Aliyezaliwa kimwili analipwa kimwili aliyezaliwa kiroho analipwa kiroho, YOHANA 4:24 , YOHANA 3:6.

Mifumo ya Mungu ya malipo ipo hapa katika maandiko yasemayo’’ Kwa sababu Mungu humpa yeye aliyemrithia Hekima, Maarifa na Furaha; bali mwenye dhambi au mkosaji humpa taabu ili kukusanya na kututa au kurundika apate kumpa huyo ambaye Mungu amrithia’’- MHUBIRI 2:26, PIA KUTOKA 23:25-25, AYUBU 36:11, MATHAYO 6:33. YOHANA 15:16, ISAYA 3:10

SEHEMU HII NI YA MAANDIKIKO MATAKATIFU:
“Hao wana amri ya kuzifunga mbingu, ili mvua isinyeshe katika siku za unabii wao. Nao wana amri juu ya maji kuyageuza kuwa damu, na kuipiga nchi kwa kila pigo, kila watakapo.” SUV UFUNUO WA YOHANA 11:6,

“Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;” SUV MITHALI 3:5,
“Kumcha Bwana ndio mwanzo wa hekima, Wote wafanyao hayo wana akili njema, Sifa zake zakaa milele.” SUV ZABURI 111:10
“Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
” SUV WARUMI 12:2,
“Tumieni akili kama ipasavyo, wala msitende dhambi; kwa maana wengine hawamjui Mungu. Ninanena hayo niwafedheheshe.” SUV 1 WAKORINTHO 15:34

“Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu. Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana” SUV WAEFESO 5:15-17,

“Enendeni kwa hekima mbele yao walio nje, mkiukomboa wakati.” SUV WAKOLOSAI 4:5
“Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana” SUV JOSHUA 1:8
“Na roho ya Bwana atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha Bwana;” SUV ISAYA 11:2

“Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.” SUV MATHAYO 6:33

“Muda nchi idumupo, majira ya kupanda, na mavuno, wakati wa baridi na wakati wa hari, wakati wa kaskazi na wakati wa kusi, mchana na usiku, havitakoma.” SUV MWANZO 8:22
“Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo. Akuambia, Haya, kula, kunywa; Lakini moyo wake hauwi pamoja nawe.” SUV MITHALI 23:7

“Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.” SUV YOHANA 4:24 ,

“Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.” SUV YOHANA 3:6
“Kwa sababu Mungu humpa yeye aliyemridhia hekima na maarifa na furaha; bali mkosaji humpa taabu, ili kukusanya na kututa, apate kumpa huyo ambaye Mungu amridhia. Hayo nayo ni ubatili na kujilisha upepo.” SUV MHUBIRI 2:26,

“Kama wakisikia na kumtumikia, Watapisha siku zao katika kufanikiwa, Na miaka yao katika furaha” SUV AYUBU 36:11,
“Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni.” SUV YOHANA 15:16,

“Waambieni wenye haki ya kuwa watakuwa heri, kwa maana watakula matunda ya matendo yao” SUV ISAYA 3:10

SALA YA YA TOBA
YESU MWANA WA DAUDI…X3
Mimi “Taja Majina yako Mawili”
NAOMBA UNIREHEMU…X3
Unisamehe Makosa Yangu Yote,
 Unisamehe Dhambi Zangu Zote,
Unisamehe Maovu Yangu Yote,
Uniponye na Magonjwa Yangu Yote
Unisafishe Kwa Damu Yako Takatifu,
Kuanzia Leo,
Ninakiri,
Nimekua Kiumbe Kipya,
Ya Kale Yamepita,
Futa Jina Langu,
Katika Kitabu Cha Mauti,
Andika Jina Langu Katika,
Kitabu Cha Uzima,
Asante Mungu,
Kwa Kunipenda,
Asante Yesu Kristo,
Kwa Kuniokoa,
Asante Roho Mtakatifu,
Kwa Kunifundisha,
Asante Malaika Wa Mungu,
Kwa Kunilinda,
Katika Jina la Uweza la
YESU KRISTO wa Nazareti.
*AMEN*

JIBARIKI MWENYEWE
HAKIKA, MIUZIJA YA KRISTO,
ISHARA NA MAAJABU,
ZITA NIFUATA MIMI,
“TAJA MAJINA YAKO MAWILI”
SIKU ZOTE ZA MAISHA YANGU,
NAMI NINA KAA NYUMBANI MWA BWANA,
MILELE NA MILELE.
*AMEN*

MASOMO HAYA YANATOLEWA BURE KATIKA OFISI ZETU ZA ARUSHA WASILIANA NASI
 +255 788 71 56 56

SHIRIKISHA WENGINE  BARAKA HIZI  UPATE KUBARIKIWA NA WEWE.
                                               MWANZO 12:1-3


1 comment:

              2021-MWAKA WA AKILI INAYOPITA MIPAKA Kingdom Business Clubaship  leo Tumeingia Mwaka 2021, Kila Mwaka Tarehe Moja Ya Mwezi Wa ...