Friday, June 9, 2017

Life is a Team



  • 5th June, 2017.
  • THE LOVE OF GOD AND PEOPLE (Mathayo 22:36-40)
  • KINGDOM JOBS (Mathayo 9:36-37)
  • TIME & BUSINESS COACH
  • Title: THE TEAM LEADER
  • Mathayo 1:21

Subtitle: LIFE IS A TEAM, Mwanzo 1:26-28, Mwanzo 2:18

Unapoenda kutafuta kazi au ajira utaulizwa kiongozi wako ni nani? Ama wataendelea kukuukiza nani unamfahamu “who is your referee” ili upate kazi hii? ni nani anaye kusababishia upate kazi? Kama ni mtu unamtegemea upate kazi kupitia mtu huyo ujue  kazi hiyo ni ya mda mfupi tu lakini kama ni Yesu mtegemee Yesu; na ukimtegemea Yesu ujue kazi hiyo ni ya mda mrefu Daniel 11:32 kwa kadri unavyo mfahamu mtu fulani ndivyo watakavyo kuamini na kukupa kazi hiyo. Wewe kama mkristo kiongozi wako ni nani?

Maisha ni timu-timu hii inaanzia watu wawili kama ilivyo mke na mume(Mwanzo 2:18), huwezi ukawa mwenyewe kama unataka kufanya biashara au kazi tambua timu inaanza na watu wawili na kuendelea…jiulize ni nani wewe upo naye kwenye timu yako? Na ukikutana na timu mbaya au umechagua timu mbaya itakuharibia maisha yako! 

Mdaraja katika Timu,
Kuna madaraja saba katika timu, ili uonekane kiongozi lazima uanzie kuongoza mahala fulani kwa kupitia hilo utakua katika madaraja haya. Mdaraja hayo ni;

1   A Home-Class Team, kwa mfano Daudi
2    A School-Class Team, kwa mfano katika Taaluma, michezo n.k
3     A Church-Class Team, jifunze kuwa daraja la kwanza “study always on first class “A”
4     A Street-Class Team, Yesu alikuwa mwalimu Luka 4:18 “Kuna ‘A’ za barabarani na ‘A’ za Shuleni”
5    A World-Class Team, mtu maarufu yeyote yule Duniani alianza chini-Askofu Oyedepo
6     A Heaven-Class Team, Jiambie lazima Mbingu ufike baada ya maisha haya
7     A Jesus-Class Team, Petro alijua kutengeneza daraja lake “his Class”, alijiachia kwa Yesu Mazima kwa maana alikuwa na shauku kubwa ya kumtumikia Yesu Kristo. Yohana 21:15-17, Yesu alimkabidhi Petro majukumu.

Jiulize wewe leo “which one is your class” na umeiweka pamoja na kuitengenezea wapi? Na ikumbukwe ya kuwa Timu ya Kristo ni Mathayo 6:33. Katika huduma hii tunawafundisha watu kujitegemea wenyewe siyo kuwafuata fuata na kuhama hama unapo abudu eti ukitafuta ‘maombi’ au nguvu za Mungu/ishara kwani maandiko yanasema katika Yeremia 3:15, jitegemee kuwa mfuasi na mwanafunzi  wa Yesu Kristo.

Jifunze na uanze kutoka uliko ili usonge mbele kutoka “class team” kwenda “Team Leader”, kwa kuwa kwenda kufanya kazi ya Mungu haikuzuii kufanya Biashara zako zingine kwa mfano Askofu David Oyedepo ana makampuni Zaidi ya 30 ya kibiashara kama watu wengine wa kawaida. Unapo anza kufanya kazi ya Mungu kazi hii itakusaidia kupata wateja wengi. Hakuna baishara isiyo hitaji watu, na watu ndiyo bidhaa ya bure tena ina patikana kila mahali ukianzia barabarani. Tafadhali kumbuka ya kuwa ili ufalme ukamilike unahitaji watu hakuna falme bila watu, Yohana 15:16.

HITIMISHO
Zaburi 84:7, 2 Wakorintho 3:18, “From Class Team to Team Leader”
Usisahau ya kuwa maisha ni Timu na huwezi kukaa mwenyewe pasipo kuanza na mtu mwingine.

Unaswali/Maoni/Mapendekezo komenti hapo chini au Una ushuhuda usisite kutuandikia Kupitia hapa au kwa rewiew section ya Facebook (Tazama kwenye ukurasa huu utaziona nyota hivi, ziweke upendazo baadae andika hapo-Asante.)

No comments:

Post a Comment

              2021-MWAKA WA AKILI INAYOPITA MIPAKA Kingdom Business Clubaship  leo Tumeingia Mwaka 2021, Kila Mwaka Tarehe Moja Ya Mwezi Wa ...