JINSI YA
KUTENGENEZA AJIRA SEHEMU YA TATU
Salamu!
Yesu Mwana wa
Daudi, Hallelujah x3
"BADILISHA
MUDA KUWA AJIRA NA GEUZA AKILI KUWA HEKIMA"
UFUNUO WA YOHANA
11:6, MITHALI 3:5, ZABURI 111:10
WARUMI 12:2,
1WAKORINTHO 15:34
Tajirika Na Muda –Tumia Muda
Kibiashara
Waefeso 5:15-17, Wakolosai 4:5
Mungu amempa
Mwanadamu uwezo mkubwa sana. Mwanadamu anaweza kugeuza Muda kuwa chochote
anachotaka kwa kufikiri kwa kina. ‘’Hapo Mwanzo Mungu aliziumba Mbingu na
Nchi’’ -Mwanzo ni Muda- ‘’KUTAFAKARI’’
ZABURI1:1-3
JOSHUA 1:8 UFUNUO 11:6
Mwanadamu anaweza
kugeuza akili kuwa pesa. Mungu alimpa Sulemani Hekima akaigeuza akili kuwa
Utajiri.
Kugeuza akili
kuwa Hekima ni kubadili akili kuwa vitu. Mawazo ni vitu Geuza Mawazo yako kuwa
Sayansi ,Tekinolojia Ufundi, Vitabu, Semina, Sinema na DVD;s, CD’s nk.
Hekima ni kitu
cha mwisho, ukiona Magari ya aina ya Toyota ni Hekima ya MJAPANI – ‘’Japanese
Wisdom’’.
Katika Roho Saba
za Mungu, Nne zinahusiana na Hekima. Roho ya ufahamu ni Hekima, Roho ya Ushauri
ni Hekima, Roho ya Maarifa ni Hekima na Roho ya Hekima ni Hekima. Ukigeuza
Akili kuwa Hekima huwezi kushindwa mahali popote Duniani na Mbinguni-ISAYA11:2
Ukitengeneza
ajira kivuli utapata faida kivuli na faida kivuli inatengeneza faida hasili.
Ajira kivuli ni kazi za Kijamii, Ukipanda Mbegu ya Kazi utavuna Matunda ya
Kazi. Ajira ni kama nyumba huwezi kujenga nyumba bila kuwa na Ramani ya jengo. Ramani
ni nyumba kivuli.
Anza kidogo
kidogo mwenyewe na Muda wako wa masaa 24Hrs mpaka ufikie kiwango cha Kugeuza
Muda kuwa Ajira. Wewe unafikiri wengine wanafanya kazi.
Ajira kivuli
ndiyo jibu la kila Mtanzania na Dunia kwa ujumla. Ramani ya Ajira ni kazi za
kijamii-MATHAYO 6:33
Ajira kivuli ni
Kazi ya Yesu, Kazi ya Adamu na Kazi ya Injili.
Kazi ya Yesu ni
kusaidia Yatima,Wajane, Wafungwa, Wagonjwa, Watoto wa Mitaani,Walemavu, Wazee
na Wasio jiweza.
Kazi ya Adamu ni
Kutunza Mazingira, Wanyama, Misitu na Vyanzo vya Maji.
Kazi ya Injili
Kufundisha Habari Njema.
KUMBUKA KWA MUNGU
HAKUNA KUJITOLEA ANALIPA KILA BAADA YA DAKIKA SITINI. "60MINS"-LISAA
LIMOJA’, UNAMCHAJI MUNGU KWA KILA LISAA LIMOJA KIWANGO UNACHOTAKA KULINGANA NA
UZITO WA KAZI UTAKAYO FANYA-MATHAYO 20:1-16
Kama unahitaji
kazi lazima utembee kwenye agano la kazi upande Mbegu ya kazi uipe muda utavuna
matunda ya kazi yako. Kila kitu unachokiona Duniani kina Mbegu, nikikupa Tsh
1000 Sasa hivi kuna mbegu ndani yake asilimia moja ambayo ni Tsh Shilling
kumi-MWANZO 8:22
Ukiona Wazungu
wana kuja Afrika kufanya kazi za kijamii kama kwenye Vituo vya Watoto Yatima,
Mashule, Hospitali, Kutunza Mazingira, NGO’s mbalimbali wamekuja kupanda mbegu
ya kazi. Mungu anataka umuonyeshe kazi ya mfano ili aweze kukutengenezea Ajira.
Kazi ya Muda ni
Kufikiri, Kutengeneza Ajira, Wazo la Biashara na Kutafuta Taarifa. Kazi ya Muda
siyo kutafuta pesa, Kazi ya pesa ni kuukomboa Muda wako. Kwa mfano Safari ya
kutoka Arusha mpaka Dar ess salaam kwa Basi ni masaa kumi , ukisafiri kwa Ndege
ni lisaa limoja kwahiyo ukipanda Ndege utakuwa umekomboa masaa tisa, Hiyo ndiyo
kazi ya pesa, WAEFESO 5:15-17, WAKOLOSAI 4:5
Mimi nimebadili
Muda wangu kuwa ajira na nimegeuza Akili yangu kuwa Pesa. Kila mtu anaweza
kufanya kama nilivyo fanya mimi, 1 WAKORINTHO 15:34
Ajira yako ipo
ndani ya Muda wako na pesa zako zipo ndani ya akili yako kila mtu anao Muda wa
masaa 24hrs na kila mtu anazo akili. Akili haitengenezi Pesa mpaka ibadilike
kuwa Hekima. Sulemani alitatua matatizo ya watu kwa kutumia Hekima. Mfalme
Sulemani hakutatua Matatizo kwa kutumia Pesa kama Dunia ya Leo walio wengi
wafanyavyo. Utakapotatua tatizo la mtu kwa muda wako na akili yako atakulipa.
Akili ni rafiki
mkubwa wa muda mahali akili yako itakapo kwenda ndiko muda wako utakapo kwenda,
kitakachomea kwenye Ubongo ndicho kitakachomea kwenye moyo wako, MITHALI 23:7
MATHAYO 6:19-21
Kazi ya Akili ni
kuuza Muda kwa Faida, Akili ikishindwa kuuza Muda mtu huyo basi anaitwa
Maskini. Mungu na wanadamu wote wananunua Muda. Mungu analipa vizuri kuliko
wanadamu. Mungu ni mwaminifu sana na analipa wakati huo huo ukimaliza kazi
yake.
Watu wengi
hawajui mfumo wa Mungu anaotumia kuwalipia watu wanao mtumikia katika ufalme
wake. Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika Roho na
kweli. Watu wanajua mifumo ya kimwli tu hawajui mifumi ya kiroho. Aliyezaliwa
kimwili analipwa kimwili aliyezaliwa kiroho analipwa kiroho, YOHANA 4:24 ,
YOHANA 3:6.
Mifumo ya Mungu
ya malipo ipo hapa katika maandiko yasemayo’’ Kwa sababu Mungu humpa yeye
aliyemrithia Hekima, Maarifa na Furaha; bali mwenye dhambi au mkosaji humpa
taabu ili kukusanya na kututa au kurundika apate kumpa huyo ambaye Mungu
amrithia’’- MHUBIRI 2:26, PIA KUTOKA 23:25-25, AYUBU 36:11, MATHAYO 6:33.
YOHANA 15:16, ISAYA 3:10
SEHEMU HII NI YA
MAANDIKIKO MATAKATIFU:
“Hao wana amri ya kuzifunga mbingu, ili mvua
isinyeshe katika siku za unabii wao. Nao wana amri juu ya maji kuyageuza kuwa
damu, na kuipiga nchi kwa kila pigo, kila watakapo.” SUV UFUNUO WA YOHANA 11:6,
“Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala
usizitegemee akili zako mwenyewe;” SUV MITHALI 3:5,
“Kumcha Bwana ndio mwanzo wa hekima, Wote
wafanyao hayo wana akili njema, Sifa zake zakaa milele.” SUV ZABURI 111:10
“Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali
mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo
mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
” SUV WARUMI 12:2,
“Tumieni akili kama ipasavyo, wala msitende
dhambi; kwa maana wengine hawamjui Mungu. Ninanena hayo niwafedheheshe.” SUV 1
WAKORINTHO 15:34
“Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si
kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; mkiukomboa wakati kwa
maana zamani hizi ni za uovu. Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni
nini yaliyo mapenzi ya Bwana” SUV WAEFESO 5:15-17,
“Enendeni kwa hekima mbele yao walio nje,
mkiukomboa wakati.” SUV WAKOLOSAI 4:5
“Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani
mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda
sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia
yako, kisha ndipo utakapositawi sana” SUV JOSHUA 1:8
“Na roho ya Bwana atakaa juu yake, roho ya
hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha
Bwana;” SUV ISAYA 11:2
“Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki
yake; na hayo yote mtazidishiwa.” SUV MATHAYO 6:33
“Muda nchi idumupo, majira ya kupanda, na
mavuno, wakati wa baridi na wakati wa hari, wakati wa kaskazi na wakati wa
kusi, mchana na usiku, havitakoma.” SUV MWANZO 8:22
“Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo.
Akuambia, Haya, kula, kunywa; Lakini moyo wake hauwi pamoja nawe.” SUV MITHALI
23:7
“Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa
kumwabudu katika roho na kweli.” SUV YOHANA 4:24 ,
“Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na
kilichozaliwa kwa Roho ni roho.” SUV YOHANA 3:6
“Kwa sababu Mungu humpa yeye aliyemridhia
hekima na maarifa na furaha; bali mkosaji humpa taabu, ili kukusanya na kututa,
apate kumpa huyo ambaye Mungu amridhia. Hayo nayo ni ubatili na kujilisha
upepo.” SUV MHUBIRI 2:26,
“Kama wakisikia na kumtumikia, Watapisha siku
zao katika kufanikiwa, Na miaka yao katika furaha” SUV AYUBU 36:11,
“Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi
niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu
yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni.” SUV
YOHANA 15:16,
“Waambieni wenye haki ya kuwa watakuwa heri,
kwa maana watakula matunda ya matendo yao” SUV ISAYA 3:10
SALA YA
YA TOBA
YESU
MWANA WA DAUDI…X3
Mimi
“Taja Majina yako Mawili”
NAOMBA
UNIREHEMU…X3
Unisamehe Makosa Yangu
Yote,
Unisamehe
Dhambi Zangu Zote,
Unisamehe Maovu Yangu
Yote,
Uniponye
na Magonjwa Yangu Yote
Unisafishe Kwa Damu Yako Takatifu,
Kuanzia Leo,
Ninakiri,
Nimekua
Kiumbe Kipya,
Ya Kale
Yamepita,
Futa Jina
Langu,
Katika Kitabu
Cha Mauti,
Andika Jina
Langu Katika,
Kitabu Cha
Uzima,
Asante
Mungu,
Kwa
Kunipenda,
Asante Yesu
Kristo,
Kwa
Kuniokoa,
Asante Roho
Mtakatifu,
Kwa
Kunifundisha,
Asante
Malaika Wa Mungu,
Kwa
Kunilinda,
Katika Jina
la Uweza la
YESU
KRISTO wa Nazareti.
*AMEN*
JIBARIKI MWENYEWE
HAKIKA,
MIUZIJA YA KRISTO,
ISHARA NA
MAAJABU,
ZITA NIFUATA
MIMI,
“TAJA MAJINA YAKO MAWILI”
SIKU ZOTE ZA
MAISHA YANGU,
NAMI NINA
KAA NYUMBANI MWA BWANA,
MILELE NA
MILELE.
*AMEN*
MASOMO HAYA YANATOLEWA BURE KATIKA OFISI ZETU ZA ARUSHA WASILIANA
NASI
+255 788 71 56 56
SHIRIKISHA WENGINE BARAKA HIZI UPATE KUBARIKIWA NA WEWE.
MWANZO 12:1-3
amen.asante kwa mafundisho mazuri
ReplyDelete