THE LOVE OF GOD AND PEOPLE
(Mathayo 22:36-40)
KINGDOM JOBS (Mathayo 9:36-37)
TIME & BUSINESS COACH
Title: THE FRIENDS OF GOD/MARAFIKI WA MUNGU
2 Wakorintho 5:7
Waebrania 11:6,;10:38
Warumi 10:7
Zaburi 11:3
Chanzo cha mwanadamu ni Mungu kwa kuwa maandiko yanasema “Mungu akasema Na tumfanye mtu kwa mfano wetu… Mwanzo 1:26” na
akasema sisi tu miungu wadogo ndiyo maana tu marafiki wa Mungu. Yesu Kristo
alisema hatatuita tena watumwa bali marafiki- sisi tu kaka na dada wa Yesu Kristo(Waebrania 2:11-KJV),Wagalatia 4:7. Wewe ni rafiki wa
Mungu, na ili uwe rafiki wa Mungu lazima uweze kutawala na Yeye.
Ili upate kazi lazima uwe rafiki wa Mungu kwanza kama ilivyo
kwa kampuni Fulani uendapo kuomba kazi lazima umjue mtu Fulani mwenye nafasi ya
juu ili upate kazi kwa kampuni hiyo. Kama baba yako hakuwa na jina kubwa nchini
au eneo uishilo ni vigumu kupata kazi ndiyo maana lazima uwe rafiki wa Mungu
kwanza kabla hujaenda kwenda kuomba kazi. Kama una tengeneza urafiki wa fedha na
fedha na ikatokea ukaishiwa hakika utakufa! Ukiwa rafiki wa Yesu Kristo
hutembei na Fedha, watu wengi wana urafiki na yule mwovu kwa maana hupenda pesa
mno kuliko Mungu.
2 Wakorintho 5:7, huwezi kumpendeza Mungu kwa kuona tu kwa
kuwa ukitaka kutengeneza urafiki na Mungu vitu vyako vyote lazima vianze na kwenda kwa Imani(Kuona rohoni mwako). Watu wengi wanaoteseka duniani leo ni wale
wanaoishi kwa kuona hasa kwa mambo ya mwilini. Na ikitokea kila kitu ukitaka kufanya
mpaka uanze kwa kuona kwanza utakuwa unafanya vitu vyako kwa kiwango cha hali ya chini sana“slow
sana”
Vitu vinavyo mtenganisha mtu na Mungu ni kama ifuatavyo;
- Sin/dhambi- Warumi 6:23
- Ignorance/Ujinga- Hosea 4:6
- Fear/Hofu- 2 Timotheo 1:7
- Shame/Aibu- Waebrania 12:2
Ili uwe urafiki na Mungu lazima kwanza uanze kufanya vitu
viwili tena iwe mwendelezo;
- Repent/tubu-Mathayo 4:17, Matendo 3:19, Tafuta Mistari ya Toba, Tafuta Neno la kusimamia.
- Think through the Word of God/Fikiri kwa kupitia Neno-Joshua 1:8, Facts and Truth ndilo Neno la Mungu.
Mungu akiongea
anaumba, mwanadamu akiongea ana fikiri kupitia Neno lake (la Mungu).
Vifuatavyo ni vyanzo ya kufikiri:
- Kufikiri kupitia Neno la Mungu
- Kufikiri kupitia umbaji wa Mungu
- Kufikiri kwa Kupitia kazi ya Adamu (Mwanzo 2:15) na Kazi ya Yesu (Mathayo 1:21, 6:33) Kupitia kazi hizi mbili za Adam na Yesu utaona unaanza kuhudumiwa na Malaika. Utakapoanza kumrudishia Mungu Muda wako ndipo malaika wataanza kukuhudumia.
HITIMISHO
Aibu rafiki yake mkubwa ni hofu. Hofu na aibu siyo Imani, jifunze kujifunza kufuta dhambi mara kwa
mara ili ujinga, hofu na aibu viondoke.
Mithali 10:22, fedha chafu hununua vitu vichafu, fedha safi
hainunui vitu vichafu na mtu hatajiriki na pesa bali Baraka zitokazo kwa Mungu. Acha kutegemea nature”asili” tegemea
huduma ya Malaika…eti msimu huu ni msimu wa maembe, acha kutegemea vitu vya asili.
Unaswali/Maoni/Mapendekezo komenti hapo chini au Una ushuhuda usisite kutuandikia Kupitia hapa au kwa rewiew section ya Facebook

No comments:
Post a Comment