THE LOVE OF GOD AND PEOPLE
(Mathayo 22:36-40)
JESUS IS LORD
KINGDOM BUSINESS CLASS (Mathayo 6:33)
TIME & BUSINESS COACH
Title: THE SEED OF BUSINESS/MBEGU YA BIASHARA
LUKA 8:11
YOHANA 1:1-5
LUKA 2:49
Mbegu nini?
Mbegu ni sehemu ya chanzo cha kitu fulani inaweza
ikawa tunda la mmea ukaendelea na kuwa mmea mpya. Mbegu ni njia ya kuzaa vitu
vingi ndani ya muda kama ilivyo Mbegu ya mmea inaanzishwa ndani ya ua la mmea
inaendelea kukua na ndivyo ilivyo maisha ya mwanadamu utajiri au mafanikio yake
yapo ndani ya muda.
Mungu alipoziumba mbingu na dunia kila kitu ndani yake
aliweka mbegu siyo tu katika miti, mimea,majani na wanyama hata binadamu pia
aliweka mbegu zake ili kuendeleza uzao wa jambo husika kwa kila masaa 24
yapewayo dunia hii. Hivyo basi kitu chochote unataka kufanya duniani humu
lazima upande mbegu kwanza chini ikiwa ni ardhini, kwenye biashara au muda n.k
Lk 8:11, Yohana 1:1-15:14, swali la msingi la kujiuliza kwa
mfano unahitaji fedha nyingi uzishike mkononi mwako wewe sasa umetoa fedha
kiasi gani kwa watu wasiojiweza “NGO” kulingana na kitabu cha Yakobo 1:27? Unata
kuishi miaka mingi hapa duniani ume mrudishia Mungu masaa mangapi unapoendelea
kuishi?
Swali la msingi la kujiuliza unapandaje mbegu sasa? Mbegu
zinapandwa kwa aina mbili kuna zile unapanda shambani hizi huoza na kuota mmea
na zile ambazo unapanda kwenye akili za watu(kuwapa mafunzo kama ilivyo huduma
hii ya Kingdom Business). Mbegu hizi huwa hazifi kabisa utazivuna kwa wakati
usio jua ‘mbegu za kiroho’. Napenda utambue ya kwamba utajiri mkubwa duniani ni
ule ambao unapandwa vichwani mwa watu ‘akilini’ kupitia taarifa “information”
unazo toa kwa watu husika. Zifuatazo ni mbegu zinazo tumika hapa duniani
- The word of God/Neno la Mungu
- Time/Muda-kila masaa 24
- Project Seed/Mbegu ya Mradi
- Seed money/Mbegu ya pesa
- The seed of a Man/Mbegu ya mwanadamu
- Plants or fruits seed/ Mimea au mbegu za matunda
Katika mpangilio huu hapo juu namba moja ndiyo jambo la kwanza katika mambo yote ‘NENO LA
MUNGU’. Kupitia Neno huzaa maneno yanayoweza yakawa ni giza la yule mwovu au
Nuru ‘NENO LA MUNGU ni sawa na kusema laana au baraka. Watu wengi wanateseka
leo kwa sababu ya labda ya maneno waliyosema au waliyo nenewa na watu na wao
hawakuyatengua yakawa giza baadae ikawa laana kwao. Futa mbegu za laana ulizo
nenewa na watu au wewe menyewe ulizo jinenea na uanze kumshukuru Mungu katika
kila jambo.
WORD FOR WORD
Neno kwa Neno ni maneno ya Baraka au laana jinsi unavyo
ongea maneno mengi yakiwa ya kiovu ndivyo utakavyo jilaani mwenyewe. Nenda
kinyume na maneno kama haya:
Challenge/Changamoto=Nenda na Neno THANKSGIVING/SHUKRANI
Temporary/ya muda mfupi=Nenda na Neno Testimony/Shuhuda
Ikitokea ukaona mambo hayaendi wala haufanikiwi cha kwanza
utambue ya kuwa Mungu hampi mtu vitu viwili kwa wakati mmoja, lazima kimoja
ukiachie ili upate kingine. Kwa uwelewa tu wa haraka haraka Mungu hawezi kukupa
fedha na Muda kwa wakati mmoja. Atakupa muda ili utafute fedha au fedha atakupa
ili uukomboe muda.
Kila masaa 24 unayopewa ya siku husika ni mbegu na inatakiwa
uipande labda shambani au vichwani mwa watu. Hapa duniani watu wameletwa au
kuumbwa kwa aina mbili.
- Kuna Watu ni MBEGU na
- Kuna Watu ni MKATE
SEED AND BREAD
God doesn’t look for beggars but partners/ Mungu hatafuti
ombaomba”wa mkate” bali washirika wa kushirikiana Naye “mbegu”
Kitu cha ajabu leo hii watu wengi ni “MKATE” ijapo kuwa
waliletwa duniani kama Mbegu na si mkate. Ni kweli kabisa kuna huu mstari “Utupe
leo riziki yetu” Mathayo 6:11 Tafsiri ingine husema “Utupe leo Mkate wetu wa
kila siku” tena mstari huu husemwa kwenye Sala ya Baba Yetu. Mstari huu uliwekwa
kwa ajiri ya mtu mchanga kiroho wewe kama umekuwa kiroho sema “Utupe leo mbegu
yetu!”
SIFA ZA MBEGU
- Seed never afraid to die/ Mbegu haiogopi kufa, Yohana 12:24
- Seed produce seed/ Mbegu huzalisha mbegu
- Seed never afraid copy and paste
- Seed gives ideas to people/ Mbegu hutoa wazo kwa watu
- Seed put others first/ Mbegu huweka wengine kwanza
- Seed uses its own faith/ Mbegu hutumia imani yake yenyewe
- Mbegu haina hofu wala woga au aibu
SIFA ZA MKATE
- Mkate hua ribika kwa haraka ‘hufa’ hauna mbegu “haizalishi nyingine”
- Mkate hujari sana mambo ya mwilini,Wagalatia 5:19-21
- Mkate HAUNA VIFUATAVYO Upendo, Furaha, Amani, Uvumilivu, Utu wema, Fadhili, Uaminifu, Upole, Kiasi.
- Mkate hujari na kuweka mambo yake kuwa ya kwanza tu na si ya wengine.
- Mkate hutoa mawazo hasi pamoja na kutumia imani ya mtu mwingine
- Mkate hukopi na kupaste kutoka kwa mwingine na huogopa kufa
- Makate una hofu,uwoga na aibu
HITIMISHO
Uanzishapo biashara lazima uwe na neno litakalo leta wazo la
kuanzia nalo katika biashara yeyote ile “THE SEED OF BUSINESS” huku ukiandika
chini wazo husika. Toa muda wako ili kuzalisha fedha kwa sababu fedha na muda
ni MBEGU YA BIASHARA.
Una swali/Maoni/Mapendekezo komenti hapo chini au Una
ushuhuda usisite kutuandikia Kupitia hapa au kwa rewiew section ya Facebook (Tazama kwenye ukurasa huu
utaziona nyota hivi, ziweke upendazo baadae andika hapo-Asante.)

No comments:
Post a Comment