Wednesday, August 30, 2017

WORK BY TIME NOT BY HANDS

28th August, 2017.

THE LOVE OF GOD AND PEOPLE (Mathayo 22:36-40)

KINGDOM JOBS CLASS (Mathayo 9:36-37)

TIME & BUSINESS COACH

Title: WORK BY TIME NOT BY HANDS/FANYA KAZI KWA MUDA SIYO KWA MIKONO

# 2 Wakorintho 5:7

Fanya kazi kwa muda na siyo kwa mikono. Tasfiri ya kazi ya muda ni kufikiri, kutengeneza mawazo mapya na kutafuta taarifa kama vile usomavyo mafunzo haya sasa “unapigana na vita ya ujinga na si umaskini”. Watu wote waliofanikiwa duniani walifanya kazi kwa muda na si kwa mikono yao! Kuna aina mbili za ufanywaji wa kazi duniani
  • Kazi zinazofanywa kwa akili
  • Na kazi zinazofanywa kwa mikono
Kazi zote zinazofanywa na akili zinafanywa kwa muda na zinazofanywa kwa mikono zinahitaji vyeti tu ‘zinafanywa kwa vyeti’. Kwa kuwa kazi zote za akili hazi hitaji vyeti vya shule wala chuo bali muda tu. Kazi/ajira unayotafuta ni kazi ya aina gani ya kutumia muda(akili) au kazi ya kutumia mikono(vyeti)

Kazi za akili ni chache na haziitaji vyeti. Katika huduma hii ya Kingdom Business tunafundisha matumizi ya muda wako “kulipwa kwa muda” kwa kuwa kazi usiyotumia akili unasubiri ulipwe kwa mwezi. 2 kor 5:7,tufanye kazi kwa muda na si kwa mikono kwa kuwa imani inahusiana na akili kwa vile muda huwezi kuuona wala kuushika utauona muda kupia matokea ya vitu unavyovifanya katika muda huo.

Kazi yeyote ukifanya ukatokwa na jasho jinji ujue kazi hiyo ni ya laana au ina vichembe-chembe vya laana au kung’ang’ana! Kwa mfano utaona Mchungaji akiwa madhabahuni akitokwa na jasho jingi! Na kazi ya akili inachukua akili nyingine inaivaa mara inakuwa ya kwako Mithali 13:20-Mtu unayetembea naye ndiye anaye amua maisha yako. Kuna aina kuu mbili za kutokwa na jasho
  •  Jasho la akili (kuanzia saa 7 usiku-11 asubuhi-kufikiri,kusoma,kutafuta maarifa
  •  Jasho la uso (wakati wa mchana na hasa hutoka na wajinga tu!
Kumbukumbu la Torati 30:19, Maisha ni mtihani wa kuchagua kwa vile vitu vingi vimewekwa mbele yako kama vile mtihani wa “multiple- choice” kuna mtu anafanya maisha yake kama ‘ana ana do’ au ana fumba na kufumbua anataka mambo yatokee. Jeremia 1:5-Hii ni kazi moja ambayo Mungu alikuitia nayo, Mungu humuingizia mtu akili kupitia muingizio “ impartation” 

#Ukienda kutafuta kazi usiende na vyeti vyako! Nenda na akili yako vyeti vitafuata baadae! Kwa kuwa hata kama unavyeti ‘makaratasi mia” lakini akili(mawazo mapya) ndiyo itakayo kupa ajira/kazi. Na siku zote tumia asilimia 80 AKILI YAKO na asilimia 20 MIKONO YAKO ukiwa kazini au kibaruani. Mungu ana fikiri wewe unatumia mikono kufanya kazi.

Kama kiongozi au Bosi wa kampuni yako mwenyewe wewe unatakiwa ufikiri wafanyakazi wako wanafanya kazi kwa maana kinachouza siyo bidhaa ni wazo(kazi na biashara vinashabiriana). Kama hufikiri ajiri watu kwa ajiri ya kufikiri tu “Think Tank”.


HITIMISHO
Katika huduma hii tunakujengea uwezo wa kufikiri na siyo kuamini vyeti ulivyonavyo kuombea kazi. Akili haikui kwa umri wala kwa kuwa na vyeti vingi bali kwa maarifa yatokanayo na kufikiri kupitia uumbaji wa Mungu huku ukitumia muda na si mikono.

 Una swali/Maoni/Mapendekezo komenti hapo chini au Una ushuhuda usisite kutuandikia Kupitia hapa au kwa rewiew section ya Facebook Page Yetu  (Tazama kwenye ukurasa huu utaziona nyota hivi, ziweke upendazo baadae andika hapo-Asante.)

No comments:

Post a Comment

              2021-MWAKA WA AKILI INAYOPITA MIPAKA Kingdom Business Clubaship  leo Tumeingia Mwaka 2021, Kila Mwaka Tarehe Moja Ya Mwezi Wa ...