27th August, 2017.
THE LOVE OF GOD AND PEOPLE
(Mathayo 22:36-40)
JESUS IS LORD
KINGDOM BUSINESS CLASS (Mathayo 6:33)
TIME & BUSINESS COACH
THE ENOUGH FAITH/IMANI INAYOTOSHA
Rum 10:17
Rum 14:2
Rum 14:23
Ebr 11:1
Imani nini?
“Kuwa na Imani ni kuwa na hakika ya mambo tunayotumainia;
kusadiki kabisa mambo tusiyoyaona” Kutoka Biblia ya Habari njema. Katika Imani
kuna ngazi kuu mbili
- Kuamini Imani (KUSIKIA+IMANI+STORY= KUAMINI
- Kujua IMANI (IMANI+STORY+NAMBA”MUDA”= Ebr 4:2
Unaweza ukaamini lakini kisitokee Ila UKIJUA “Ukijua Imani”
kitu hicho kitatokea kwa vile una tumia muda “una cheza na namba baada ya
kusikia,Imani yenyewe, story yako na muda unao kipa hicho kitu mwishoe
kitatokea. Imani ni mfumo wa fedha wa mbinguni, pale fedha ikishindwa kununua
kitu fulani imani ndiyo inachukua nafasi. Unapo angalia vitu au fedha ikashindwa
angalia Imani uliyo nayo. Kwa bahati mbaya sana leo hii watu wengi
wakipungukiwa au wakiwa hawana fedha mifukoni mwao huishiwa na nguvu kila
mahali na kuona maisha yamekuwa magumu sana pasipo fedha.
Ukiwa na Imani iliyo jitoshereza shida ikitokea na imani
uliyo nayo ni kubwa ujue utashinda tu. Ukiwa huna imani hofu huingia na hofu ni
mama yake na uwoga na baba wa uwoga ni aibu. Kuna aina tatu za kiwango cha
imani
- Neno la Imani/ The word of Faith- Rum 10:17 “Mkristo mchanga”
- Karama ya Imani/ The gift of Faith- 1 kor 12(soma yote), “Watumishi wengi wapo hapa”
- Roho ya Imani/ The spirit of Faith “Roho aliyokuwa nayo Kristo-Watumishi wakubwa wanayo hii roho, wakisema vitu vinatokea.
Kiwango cha imani kikijitosheleza utakula au kunywa kila
kitu “ Watu hutofautiana: Mmoja imani yake inamruhusu kula kila kitu; lakini
mwingine ambaye imani yake ni dhaifu, hula tu mboga za majani.” Warumi 14:2(BHN).
Kiwango chako cha imani kinaamua jinsi ya kufanya maamuzi yako “the power of
decision/nguvu ya kufanya maamuzi”
Mungu hafanyi kazi na walio na ulegevu kiimani. Mtu
asiyekuwa na nguvu ya maamuzi kiwango chako cha imani hakitoshi. Kwa mfano
walio ajiriwa hawafikirii! Wameibiwa nafasi zao na mabosi wao!
THE POWER OF DECISION MAKING
#Take Risk, jihatarishe kupitia muda wako, mali zako, na
maisha yako na kama huna nguvu ya maamuzi huwezi kutoka hapo ulipo, sehemu
mojawapo ya kuanza kufanyia maamuzi tambua ya kuwa umekuja duniani peke yako na
duniani humu kuna wajinga wengi hautaeleweka unapotoa au kushare maono yako kwa
kuwa maono hayo umepewa wewe na si wao. Imani ya watu wengi haitoshi kwa sababu
wanaangalia fedha/pesa na mtu wa namna hii ameshindwa kabla hajaanza kitu.
Mthayo 11:5, Vita vya umaskini au kufanya maombi ya umaskini
huwezi ukavishinda hata siku moja, hebu angalia vizazi vyako karibia vyote
vimeshindwa kupambana na umaskini mwisho wake umaskini ume wauwa! nchi yetu
inapambana na umaskini wewe una pambana na nini? Katika kosa kubwa linalo
fanyika leo hata makanisa yana pambana na vita ya umaskini wakati mwanzilishi
wa kanisa alikuja kama Mwalimu “Rabi” kuwafundisha watu ili waondokane na
ujinga wa mababa zao “Tubuni kwa maana ufalme wa Mungu umekaribia...-tubadilishwe
nia na akili zetu”
Baba wa Taifa Mwl Julius K Nyererena kwa ujumla duniani kipindi hicho walikuwa
wanapigana na vita vikuu vitatu vya mwanzoni hapa kuanzaia namba nne ni
nyongeza ya vita tuzo pigana nazo duniani leo hii-;
- Ujinga/Ignorance
- Umaskini/Poverty
- Magonjwa/maradhi/Sickness/disease
- Madawa ya Kulenya/Drugs
- Ushoga/Homosexual
- Ugaidi/Terrorism
- Mtandao-“ya kijamii”/Internet
Hosea 4:6, Warumi 12:2, Isaya 11:2- katika zile Roho saba za
Mungu Roho nne zinausiana na akili ambazo ni Roho ya Maarifa,Hekima, Ushauri na
Ufaham. #Faith is the state of mind/Imani ina husiana na akili and #Success comes when faith is greater than time
or with good deeds the faith is greater than time. Kwa mfano unataka kupika
ugali ukaanza kupika tu na ukatambua ya kuwa unga ni mdogo utakunywa uji hakika!
#Don’t compete with people compete with time/shindana na
muda na si watu/. #Overcome your time with good characters/ uushinde muda kwa
tabia njema. #The greatest partner is your time/Muda ndiyo rafiki yako wa
karibu huwezi kuachana naye! #Time is a person with your personality, muda
unaongea- #One habit of time is dying every second, it has a human character/Moja
ya tabia ya muda una kufa kila sekunde, una tabia ya mwanadamu.
Kusoma Neno la Mungu linaongeza kiwango chako cha imani ndipo
ujinga utaondoka lakini ukipigana vita vya umaskini hakika utakufa mapema kabla
ya muda wako! Kwa kuwa Mungu hampi pesa/fedha mtu mijnga hata siku moja mpaka
upate maarifa kwanza ili uondoe ujinga “Hosea 4:6”, unataka kuwa tajiri wa mali
nyingi tatua matatizo makubwa ya watu wengi, ongeza maarifa mengi kila sekunde
upumuayo. Ukipigana na umaskini utakuwa una tafuta fedha na ukipambana na
ujinga utakuwa unatafuta pesa “kuna tofauti kati ya pesa na fedha, fedha ni
hizi za sarafu na noti tunazoziona na Pesa ni roho kwa lugha nyingine
inaonekana kwa makaratasi kama ilivyo mfumo wa benki huendeshwa kwa kutumia
makaratasi!
Kitabu cha Mhubiri 10:15(BHN), Uki kaa na watu wanaopigana
na umaskini utajikuta na wewe unapigana vita hivyo hivyo kama ilivyo vita vya
ujinga nawe utajikuta unapigana na vita vya Ujinga. Mwisho kabisa ukitaka usiwe
mzee mapema pigana vita vya ujinga lakini ikatokea unapigana na vita vya umaskini
uzee una kukaribia haraka!
HITIMISHO
Imani iliyo jitosheleza, ikatokea kama unafanya biashara “hauja
uza” unasemaje? Ukisema umelogwa au ni hila za mwovu ujue unapigana na vita vya
umaskini ondoka hapo haraka. Asilimia 80 katika maisha ya mwanadamu anafanya
kwa sababu ya tamaa za mwili na kwa asilimia 20 zilizo baki kwa kupia mapepo! Takwimu
hizi ni kwa yule asiye tumia akili ya Mungu kwa maana Mungu anaposema “tusi
zitegemee akili zetu wenyewe” ana maanisha “tutumie akili ya Mungu pekee” –usitumie
akili yako=TUMIA AKILI YAKE, kwa mfano mtu ana kwambia usilipe maana yake yeye
ata kulipia.
Unaswali/Maoni/Mapendekezo komenti hapo chini au Una
ushuhuda usisite kutuandikia Kupitia hapa au kwa rewiew section ya Facebook (Tazama kwenye ukurasa huu
utaziona nyota hivi, ziweke upendazo baadae andika hapo-Asante.)
No comments:
Post a Comment